Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya ya Geita katika idara ya misitu wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Geita baada ya kupatikana na tuhuma 30 likiwemo la kusababishia hasara kwa mwajiri wake kiasi cha shilingi milioni 229,866,400/=
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya Desidery Kamugisha ,mwendesha mashtaka wa serikali Enosi Erasto alisema kuwa mnamo mwez wa sita mwaka 2009 na mwezi wa 12 mwaka 2011 huko katika msitu wa akiba wa Geita kwa mida tofauti tofauti washitakiwa hao wakijua ni kosa la jinai na kwa maksudi walitenda makosa hayo na kusababisha hasara kubwa kwa mwajiri wao.
Mwendesha mashitaka huyo ameongeza kuwa mara baada ya kutenda makosa hayo kwa makusudi pamoja na kutenda makosa hayo hawakuweza kutoa taarifa yoyote ya ukweli kwa mwajiri wao na hivyo wakamdanganya.
Aidha watuhumiwa hao ambao ni Emanueli Mabala,Kasika Gamba,Elizakayo Yobu shuma, Alexanda Makali Masawe, Paulo Maganya, wote wakiwa ni watumishi hiyo katika wilaya ya Geita.
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo kwa mara ya kwanza kwa hakimu Kamugisha washitakiwa hawakujibu chochote kutokana na ushahidi kutokmilika na walipelekwa rumande mara baada ya kukosa vigezo vya dhamana na kesi yao itasikilizwa tena tarehe 07 mwezi wa nane mwaka huu.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin