WATANZANIA wametakiwa kuwa makini wanapotumia simu na kompyuta, kwani ndio chanzo cha matatizo mbalimbali yakiwemo ya kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Mshauri wa masuala ya teknolojia, Alex Mpompo aliyasema hayo juzi kwenye semina inayohusu teknolojia katika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Mpompo alisema matatizo yanayochangiwa na teknolojia yapo mengi ikiwamo kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Alisema vijana wengi nchini wana upungufu wa nguvu za kiume jambo linalochangiwa na matumizi mabaya ya teknolojia hivyo kuchangia familia kusambaratika.
Aliwaasa Watanzania kutotumia kompyuta kwa muda mrefu kwa kuipakata kwenye mapaja, kwani mionzi inapenya kwa urahisi katika maeneo hayo na kuathiri mbegu za kiume na kusababisha ugumba.
alisema Mpompo.
Alisema vijana wanaoongea na simu kwa muda mrefu wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza kumbukumbu na kutosikia.