Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YULE RAIS MASKINI DUNIANI ATOA TAMKO KUHUSU FIFA KUMFUNGIA SUAREZ


RAIS wa Uruguay ambaye ni rais masikini kuliko wote duniani, Jose Mujica, ameponda Kifungo cha mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez cha miezi minne alichopewa na FIFA na badala yake anahitaji msaada wa madaktari wa magonjwa ya akili.

Suarez alifungiwa miezi Minne kutojishughulisha na chochote kuhusu Soka na pia kufungiwa Mechi 9 za Uruguay baada kupatikana na hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 24.
Akiongea na Gazeti la Brazil, Folha de Sao Paulo, Rais Mujica, ambae ndie anasifika ya kuwa Rais ‘maskini’ kupita yeyote Duniani kwa uamuzi wake wa kuishi kwenye Banda la Shambani kwake badala ya Ikulu akilindwa na Polisi Wawili tu na Mbwa wake Manuela mwenye Miguu Mitatu, amesema: 
 Anatoka Familia fukara na akili yake ni miguu yake. Ni bora kumpeleka Hospitali ambako atapata msaada wa daktari wa Magonjwa ya Akili!

Rais Mujica amefafanua: 
 Ni wehu kumfungia Mtu asishiriki lolote kuhusu Soka! Hata Serikali haina mamlaka ya kumzuia Mtu asiingie Uwanja wa Mpira bila kupata Saini ya Jaji! Lakini FIFA wanakuja wanamfungia Miezi Minne bila hata kuwa na Jopo la Kisheria!
Hivi sasa Suarez ameihama Klabu yake Liverpool ya England na kutua Barcelona ya Spain.

Na Rais Mujica amenung’unika:
 Sasa tutamuona Suarez akicheza pamoja na Neymar na Messi lakini sijui lini itakuwa hivyo!
Unadhani kwa kosa alilolifanya adhabu yake ilikua ni kumpeleka hospitali na si kufungiwa?

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com