Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wakazi wa Jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake jana wameshikwa na butwaa mara baada ya kumsikia mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kumi akielezea namna alivyobakwa na mzee mwenye umri wa miaka hamsini huko Mbezi Makabae.
Tukio hilo ambalo kwa mara ya kwanza liliruka jana kwenye kituo cha 93.7 E-FM RADIO lililotokea Ijumaa iliyopita na kulipotiwa kituo cha polisi Mbezi Makabe na kupewa jarada namba MKB/RB/232/2014 .
Muda mfupi baada ya tukio hilo E-FM ilifika kushuhudia umati mkubwa wa wananchi wenye ghazabu ambao walitangaza kiama cha kumsaka mtuhumiwa ambaye mara baada ya kutenda kosa hilo alikimbia huku Jeshi la Polisi likimtafuta kwa udi na uvumba.
Social Plugin