Habari zilizotufikia katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni
kwamba kuna mapigano makali yanaendelea kati ya wafugaji wa kabila la wataturu
kutoka wilayani Meatu na wamasai wa Ngorongoro katika kijiji cha Kakesio,Ngorongoro.
Chanzo cha mapigano kinadaiwa kuwa ni Wamasai kuiba ng’ombe za Wataturu.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mmasai mmoja na mtaturu wamepoteza maisha katika
mapambano hayo.
Imeelezwa kuwa polisi wa Meatu wakiongozwa na ocd wako eneo la tukio
pamoja na polisi wa Ngorongoro.
Hadi sasa hali si shwari.
Inaarifiwa kuwa licha ya polisi kutumia mbinu za kijeshi kutafuta suluhu wamang'ati au wataturu wanataka wapewe ng'ombe zao na si vinginevyo.
Inaarifiwa kuwa licha ya polisi kutumia mbinu za kijeshi kutafuta suluhu wamang'ati au wataturu wanataka wapewe ng'ombe zao na si vinginevyo.
Na Samwel Mwanga -Simiyu