Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News!! MAPIGANO MAKALI KATI YA WAFUGAJI WA KITATURU NA WAMASAI HUKO NGORONGORO YANAENDELEA HIVI SASA ,INAELEZWA MPAKA SASA KUNA WALIOPOTEZA MAISHA

Habari zilizotufikia katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba kuna mapigano makali yanaendelea kati ya wafugaji wa kabila la wataturu kutoka wilayani Meatu na wamasai wa Ngorongoro katika kijiji cha Kakesio,Ngorongoro.

Chanzo cha mapigano kinadaiwa kuwa ni Wamasai kuiba ng’ombe za Wataturu.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mmasai mmoja na mtaturu wamepoteza maisha  katika mapambano hayo.

Imeelezwa kuwa polisi wa Meatu wakiongozwa na ocd wako eneo la tukio pamoja na polisi wa Ngorongoro.
Hadi sasa hali si shwari.

Inaarifiwa kuwa licha ya polisi kutumia mbinu za kijeshi kutafuta suluhu wamang'ati au wataturu wanataka wapewe ng'ombe zao na si vinginevyo.

Na Samwel Mwanga -Simiyu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com