Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GARI LILILOBEBA MAITI 10 LAUA WATU WAWILI MKOANI MOROGORO

 Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Land Cruser lililokuwa imebeba maiti 10 zikitokea hosiptali ya taifa Muhimbili kwenda hospitali ya St Francis Ifakara kugonga wapanda pikipiki katika eneo la Mtego wa simba Mikese mkoani Morogoro
Akizungumzia tukio hilo kwenye  eneo la tukio mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifasi Mbao amesema gari hiyo ikiendeshwana dereva Pankrasi Pasco mkazi wa ifakara iliwagonga wapanda pikipiki Shaban Rajab na Ally Benulo wakazi wa Mikese na kufariki dunia papo hapo.

 Chanzo cha ajali  mwendo kasi na dereva anashikiliwa na jeshi la polisi, kuhusu maiti 10 zilizokuwemo katika gari hiyo amesema zilikuwa zikipelekwa hospitli ya St Fancis Ifakar kwa lengo la kufanya utafiti na mafunzo ambapo wanafanya mawasilino ya kuzifikisha katika hospitali hiyo.

Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo  kasi huku wakilalamikia matukio ya ajali nyingi katika eneo hilo kutokana na kona na kuomba serikali kuweka matuta  na vibao vya tahadhari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com