Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Kwa mujibu wa BBC Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.
Taarifa kuhusu mtu huyo anayedhaniwa kuwa na virusi vya ebola imekuja huku hofu ikiendelea kutanda katika maeneo mbalimbali na juzi mkoani Shinyanga wauguzi na madaktari walitumua mbio baada ya kupokea mgonjwa aliyekuwa anatokwa damu puani na mdomoni,ingawa hata hivyo uchunguzi ulionesha kuwa hakuwa na Ebola
BOFYA HAPA USOME KUHUSU HOFU YA EBOLA ILIYOZUA BALAA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA
Social Plugin