Hatari kweli_MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TREKTA SHINYANGA


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ester Marco (28-30) amefariki dunia baada ya kugongwa na Trekta katika barabara a Kahama kuelekea Masumbwe eneo la kijiji cha Shunu kata ya Nyahanga wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Agosti 5 ,mwaka huu saa 12 na nusu asubuhi ambapo Trekta lisilojulikana namba za usajili wala mmiliki wake likiendeshwa na dereva asiyejulikana jina wala makazi yake lilimgonga mwanamke huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda Kamugisha alisema mwanamke huyo alikuwa anatembea kwa miguu katika barabara hiyo na baada ya ajali hiyo kutokea dereva alitoweka na trekta hilo.


Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa trekta hiyo na kwamba juhudi za kumtafuta dereva na trekta hilo zinaendelea.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post