Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Ester Marco
(28-30) amefariki dunia baada ya kugongwa na Trekta katika barabara a Kahama
kuelekea Masumbwe eneo la kijiji cha Shunu kata ya Nyahanga wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP
Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Agosti 5 ,mwaka huu saa 12 na nusu
asubuhi ambapo Trekta lisilojulikana namba za usajili wala mmiliki wake
likiendeshwa na dereva asiyejulikana jina wala makazi yake lilimgonga mwanamke
huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda Kamugisha alisema mwanamke huyo alikuwa
anatembea kwa miguu katika barabara hiyo na baada ya ajali hiyo kutokea dereva
alitoweka na trekta hilo.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa trekta
hiyo na kwamba juhudi za kumtafuta dereva na trekta hilo zinaendelea.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin