Mjumbe wa bunge maalum la katiba kutoka kundi la 201,Thomas Magnus Mgoli amelazwa katika hospitali ya mkoa Dodoma baada ya kupigwa na wanaodaiwa kuwa 'vijana ambao mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)'.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa kitandani kwake, Mgoli amesema alishambuliwa na vijana hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D anakoishi.
Amesema vijana hao hukutana nao mara kwa mara anapokwenda dukani na huzungumzia masuala ya bunge hilo, lakini hiyo jana walimshambulia kwa kumuambia kuwa yeye ni CCM.
Pichani waziri mkuu aliyejiuzulu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mh Mgoli hospitalini hapo, wote wako kamati moja.
via>>FikraPevu
Social Plugin