HAYA NDIYO MAMBO MAKUBWA YANAYOFANYWA NA SHIRIKA LA EGPAF NA AGPAHI MKOANI SHINYANGA
الجمعة, أغسطس 15, 2014
Hapa ni ndani ya ofisi ya kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga Dkt John Fabian Ng'home(pichani).
Hapa anazungumza na waandishi wa habari walioambatana na mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda katika ziara yake ya siku 4 mkoani Shinyanga,kufanya tathamini kuhusu miradi inayosimamiwa na shirika hilo mkoani Shinyanga,ambapo anakutana na wataalam wa afya na wananchi walionufaika kupitia shirika hilo, AGPAF ni shirika linalojihusisha na kutokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto likifadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la USAID na CDC.
Dkt Ng'home alisema hospitali ya wilaya ya Kahama ni miongoni mwa vituo vitatu(vingine ni hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya cha Nindo) mkoani Shinyanga vinavyosaidiwa na EGPAF na AGPAHI kuhusu huduma ya uzazi wa mpango,uchunguzi kuhusu saratani ya shingo ya kizazi na kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kulia ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri ya mji Kahama Jerome Onesmo ambaye alisema mwitikio wa akina mama kufika katika hospitali ya wilaya ya Kahama ni asilimia 100 kwani kila siku wamekuwa wakipokea akina mama zaidi ya 40 wanaofika kupima afya zao kwa hiari huku akipongeza kazi nzuri ya EGPAF na AGPAHI katika kusaidia jamii kwani wamekuwa wakitoa pia vifaa tiba kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na uzazi wa mpango.
Kushoto ni mratibu wa kudhibiti UKIMWI katika halmashauri ya mji wa Kahama Dkt Ayamery Mlay akizungumzia kuhusu mkakati wa kutokomeza maambukizai kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambapo alisema kila mjamzito akifika katika hospitali kwa mara ya kwanza hupimwa vvu na akibainika kuwa navyo basi huanzishiwa matibabu/chanjo mara moja ili kumkinga mtoto asiambukizwe.
Dkt Ayamery Mlay alitumia fursa hiyo pia kuwataka akina mama kuacha kujifungulia majumbani na kwa wakunga wa jadi huku akieleza changamoto kubwa inayowakabili sasa kuwa ni upatikanaji wa damu salama.
Ziara inaendelea_Hapa ni ndani ya Jengo la Afya ya Uzazi katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
Wataalam wa afya ya uzazi wakizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,uzazi wa mpango pamoja na mkakati wa kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.Waliliomba shirika la EGPAF na AGPAHI kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa afya na kutoa vifaa tiba kwani mji wa Kahama umekuwa na mwingiliano wa watu wengi na wengi wamekuwa wakifika katika hospitali hiyo na kujikuta ikizidiwa kwa kuwa na wateja wengi
Kushoto ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri ya mji Kahama Jerome Onesmo akisistiza kuhusu umuhim wa wanaume kwenda na wake zao/wenza wao katika hospitali na vituo vya afya(Kahama viko 17),ingawa aliiomba serikali na wadau kuongeza idadi ya vituo vya afya katika wilaya hiyo.Kulia kwake ni mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF Mercy Nyanda
Wataalam wa afya wakiwemo wauguzi na wakunga ambao walisema wamekuwa wakipokea wateja wengi ukilinganisha na idadi ya watumishi waliopo
Kushoto ni mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda akiwa na waandishi wa habari Herman Meza(The Guardian) na Grayson Kakuru(TBC) ndani ya jengo la kitengo cha afya uzazi
Hapa ni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga_Kulia ni mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda akiwa na bi Fatuma Said mkazi wa Ndembeza katika manispaa ya Shinyanga ambaye amenufaika na mradi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi unaosimamiwa na EGPAF na AGPAHI kwa hisani ya watu wa Marekani kupitia shirika la USAID na CDC.
Ziara katika Kituo cha afya cha Nindo wilaya ya Shinyanga_Kituo cha afya cha Nindo ni miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,mbali na hospitali ya mkoa wa Shinyanga na hospitali ya wilaya ya Kahama vikisimamiwa na AGPAF na AGPAHI wakishirikiana na serikali.Lakini hapa Nindo huduma za uzazi wa mpango na kuzuia maambukizi ya vvu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto zinapatikana katika kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na afya njema
Mwandishi wa habari Anceth Nyahore gazeti la Nipashe (katikati) akizungumza na akina mama katika kituo cha afya cha Nindo waliofika hapo kwa huduma mbalimbali za afya ikiwemo uzazi wa mpango
Kushoto ni mwandishi wa habari Shaaban Alley Star tv akifanya mahojiano na bi Rosemary ambaye alisema wanaume wengi wana uelewa mdogo kuhusu uzazi wa mpango hali ambayo inachangia kuongezeka kwa watoto katika jamii.Hata hivyo alisema wanawake wengi sasa wameelimika na wameanza kutumia uzazi wa mpango japokuwa kwa siri ili waume zao wasijue na kujikuta wakiachika kwani wanaume wengi wanapenda wake zao wazae kila mwaka
Waandishi wa habari pamoja na mratibu wa kitengo cha mawasiliano na utetezi shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) Mercy Nyanda (kulia) wakizungumza na wakazi wa kijiji cha Busombo/Iselamagazi wilaya ya Shinyanga kuhusu masuala ya uzazi wa mpango na changamoto wanazokabiliana nazo
Social Plugin