Kushoto ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Alex akimkabidhi hati ya heshima mbunge wa jimbo la Solwa mkoni Shinyanga mheshimiwa Ahmed Salum kwa mchango wake mkubwa katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi /kuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Solwa.mkoani Shinyanga.Edward Alex alisema mheshimiwa Salum anastahili kupongezwa kwa kazi nzuri anazozifanya katika jimbo hilo katika kuwaletea maendeleo wananchi tofauti na wabunge waliopita kwenye jimbo hilo .Hati hiyo amekabidhiwa juzi mkoani Shinyanga
Hii ndiyo hati maalum aliyokabidhiwa mbunge wa Solwa mheshimiwa Ahmed Salum
Mbunge Ahmed Salum akiwahutubia wananchi wa jimbo lake
Mheshimiwa Ahmed Salum akicheza na wananchi wake
Mbunge huyo akizungumza na wananchi wa Didia hivi karibuni |
Mbunge akiwajibika jimboni kwake
Mbunge Ahmed akiwa na viongozi wa CCM taifa katika kata ya Solwa jimbo la Solwa |
Mbunge wa solwa Ahmed Salum,aliyevaa kofia akiwa na madiwani wake wakicheza ngoma ya jeshi la sungusungu wakati wa kukabidhi madawati 77 katika shule ya msingi Bubale iliyopo kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga hivi karibuni
Social Plugin