Miongoni mwa mapambo yanayotumika zaidi na wanawake huku umaarufu wake ukiongezeka siku hadi siku ni urembo aina ya vikuku, ambavyo huvaliwa miguuni.
Awali urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.
Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.
Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.
Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao ni wadau wa urembo wanafafanua kuwa pambo hilo halina maana yoyote livaliwapo kwenye miguu ya mwanamke zaidi ya urembo kama ilivyo kwa hereni na mikufu.
anasema Nice Siema
Anafafanua kuwa uvaaji wa urembo huo hauwezi kutafsiri tabia ya mtu kwa kuwa ni pambo kama yalivyo mapambo mengine yanayotumiwa na wanawake.
anasema Siema
Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.
Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.