|
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakichota maji ukiwa ni mradi wa ziwa victoria ambao umesababisha watu wanne wajumbe wa kamati ya maji iliyokuwa ikisimamia mradi kufikishwa mahakamani kutokana na ubadhilifu wa shilingi milioni nane ambazo zinatokana na mauzo ya maji.
Hata hivyo afisa mtendaji wa kijiji hicho Paschal Chuma naye amesimamishwa kazi kutokana na uzembe pamoja na kushindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi yatokanayo na mradi huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008. |
Katika mradi huo wa maji inadaiwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kuwa kwa mwezi walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi millioni 1.6 katika kituo kikubwa na kituo kidogo ni kiasi cha shilingi millioni 1.5, lakini katika akaunti ya benki kulikuwa na kiasi cha shilingi laki tatu tangu mradi huo ulipozinduliwa mwezi wa tano mwaka 2008.
via Stella blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com