DIWANI wa kata ya Nzera wilayani Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Geita Joseph Musukuma ameibua tuhuma nzito dhidi ya halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya kubaini ubadhilifu wa pesa za wananchi kiasi cha shilingi bilioni 3.7 zilizokuwa zimetengwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji ,afya na huduma zingine.
Tuhuma hizo amezianika juzi katika baraza la madiwani la halmashauri hiyo baada kueleza katika baraza hilo diwani huyo kuwa taarifa za mkaguzi na mdhibiti wa fedha za serikali alipofanya ukaguzi maalumu mwaka jana aliokuwa ameombwa kwa mda mrefu alibaini kiasi hicho kuwa kimetafunwa na wachache katika halmashuri hiyo kati ya mwaka 2010,2011 na 2012.
Aidha diwani huyo aliongeza kuwa baada ya ukaguzi kufanyika vitabu vililetwa viwili vya taarifa hizo kimoja ni cha kiingereza na kingine cha Kiswahili lakini cha ajabu kile cha Kiswahili kilichokuwa kwa mwenyekiti kilikuwa kwa ajili ya madiwani ili wakisome vizuri na cha kiingereza kilikuwa cha mkurugenzi lakini cha ajabu cha madiwani kitabu kilipotea kwa mazingira ya utata na kubaki cha kiingereza kitabu ambacho kingeweza kuwapa shida baadhi ya madiwani kukitafasiri na hivyo kutafasiliwa huenda ilikuwa ni njama za kukipoteza kitabu hicho ili wasikione na kuhoji, alisema diwani huyo.
Madiwani hao kwa kauli moja walimtaka mkurugenzi kuwapatia tarifa hiyo na waipitie kabla ya kikao cha tarehe 4 mwezi ujao ili watoe uamuzi wa kuwawajibisha wanaotuhumiwa katika ukaguzi huo wa fedha hizo.
Hata hivyo baadhi ya madiwani walionekana kutoifahamu tuhuma hiyo kwani imekuwa ni ya mda mrefu hivyo wakataka haraka na mapema iwezekanavyo waitwe na kupewa taarifa hiyo kwa ajili ya kuijadili kwa faida ya wananchi wao.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Geita Dunkan Thebas ambaye ni afisa mipango alikiri kuwepo kwa ukaguzi katika halmashauri hiyo na kutamka mbele ya baraza hilo kuwa watapewa taarifa madiwani hao mapema iwezekanavyo ili wapate mda wa kuijadili kabla ya mwezi ujao watakapoitwa katika baraza maalumu kwa ajili ya kuitolea maamuzi.
Kwa upande wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Elisha Lupuga alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikataa na kusema kuwa’’ diwani huyo wa nzera hajasema ukweli kuhusu taarifa hiyo ni kweli ukaguzi maalumu ulifanyika na ulilenga kukagua mwka 2010,2011 na 2012 na kwa hiyo hadi sasa hivi taarifa hiyo bado ni siri na iko kwenye kamati ya fedha hadi hapo mwezi ujao tutakapokaa ili kuwaapa tuhuma wazijibu hoja zilizoainishwa humo sasa yeye amezijuaje na hizo bilioni 3.7 huoni kuwa hizo ni fedha nyingi sana karibia bajeti ya wilaya kabisa’’alisema mwenyekiti huyo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita
Social Plugin