Sababu ya kufukuzwa kwa wanahabari katika kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Misungwi,imewekwa hadharani imebainika kuwa kuna siri kubwa nyuma ya tukio hilo.
Kufukuzwa kwa waandishi wa habari Antony Sollo ,Valence Robert na Twallad Salum waliokuwa wamehudhuria kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Jumamosi Agosti 2 mwaka huu,kimetokana na Kaimu Afisa Habari Thomas Lutego kutumwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Nathan Mshana ili kuficha maovu yanayofanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Imedaiwa kuwa Lutego na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nathan Mshana wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu na Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Twallad Salum baada ya Mwandishi huyo kufichua maovu yanayofanywa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Lutego amekuwa jeuri, na amekuwa akichagua waandishi wa habari watakaofika katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa maelekezo toka kwa Mkurugenzi Mshana ili kuripoti wanachotaka wao,na si hali halisi ya matukio yanayofanyika katika halmashauri hiyo.
“ unajua halmashauri yetu imekuwa na matukio mengi ya kifisadi,sasa wakiruhusu wanahabari wengine wafike kuyaripoti siri zinaweza kuvuja matokeo yake inaweza kuleta matatizo katika utendaji na kuathili kundi linalolengwa kufichiwa maovu yake.”kilisema chanzo cha taarifa hizi”
Moja ya madudu yanayokingiwa kifua na kufichwa ili yasijulikane ni tukio la wizi wa mafuta ulifanywa na Dereva George Sanga ambaye ni mtoto wa Diwani wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi Beatrice Kaburule ambaye ni mjumbe wa kamati ya Ukimwi baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Imedaiwa kuwa sakata la wizi wa mafuta lita 290 uliofanywa na Sanga,umepelekea kumkandamiza Dereva Justine Malimi ambaye imedaiwa kuwa wakati wizi huo unafanywa alikuwa mgonjwa lakini hadi sasa ametolewa kafara kwa ajili ya kumlinda Sanga ambaye ni mtoto wa Diwani huyo ili aendelee na kazi katika halmashauri hiyo.
“Sakata hili kwa sasa lina limepewa sura ya kisiasa ili kuuficha ukweli wa mambo yanayoendeshwa hapa Misungwi, Malimi amehusishwa na wizi wa mafuta lakini kila kitu kiko wazi mhusika wa wizi wa mafuta lita 290 tunamfahamu,ni George Sanga”alisema Dereva mmoja wa Halmashauri hiyo na ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usalama wa kibarua chake.
Taarifa zimeendelea kumiminika kuwa Beatrice amejinufaisha kwa kuweka mradi hewa wa kuku hapo kwake na imedaiwa kuwa alichota fedha za mradi na kuweka kwenye mradi wake ambapo kuna banda la kuku lakini hakuna hata kuku mmoja kama inavyodaiwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Nathan Mshana kutifuana na Mwandishi wa gazeti Mwananchi Twaladi ni baada ya kuripotiwa kwa mradi hewa wa kuku 60 wenye thamani ya shilingi mil 10,000,000 ambapo Mshana alidanganya kuwepo kwa mradi huo hewa ambapo wanahabari walifika na kukuta hakuna kuku hata mmoja.
Baada ya Twallad kuripoti ukweli huo ikawa ndiyo chanzo cha mgogoro huo kati yake na kuingiliwa na Kaimu Afisa habari huyo,ambapo hadi sasa haaliki waandishi wa maeneo ya Misungwi kwa kuwa wanajua siri nyingi zainazotendeka katika Halmashauri hiyo.
Lingine kubwa kabisa ni kutafunwa kwa fedha za ujenzi wa jengo la utawala katika Halmashauri hiyo kiasi cha shilingi Mil 900.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi aliomba fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala,fedha hizo zilikuja kwa awamu ambapo mwaka 2007 /2011 waliletewa shilingi mil 600,000,000 ambazo walizitumia kwa shughuli nyingine.
Kaimu Afisa habari aliwaambia waandishi hao kuwa hawaruhusiwi kuingia katika kikao cha Halmashauri hiyo kwa kuwa si wahusika.
Imeelezwa kuwa waandishi hao waliwaona viongozi mbalimbali wakimwemo Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Khalid Mbitiyaza n Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ili waingilie kati mgogoro huo ambapo Mbitiyaza aliahidi kulifuatilia suala hili.
Mpaka sasa taarifa zilizopatikana kutoka chanzo cha habari hizi ni kwamba kutakuwa na kikao cha dharula ili kuzungumza na Mkurugenzi pamoja na baadhi ya wahusika ili kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Social Plugin