Mtoto mwenye umri wa miaka sita amefariki baada ya kukanyagwa na gari la mamake.
Bolutito Shodipe mwenye umri wa miaka sita aligongwa na mamake aliyekuwa anajaribu kuegesha gari lake nje ya kituo cha treni cha Hounslow West Tube nyakati za asubuhi Jumatano wiki hii.
Juhudi za kuokoa maisha ya Bolitito katika eneo hilo ziliambulia patupu kwani alisemekana kuaga dunia alipofikishwa hospitalini.
Taarifa kutoka kwa familia ya Bolitito ilisema kuwa wanajaribu kuikubali hali iiliyowakuta kutokana na ajali hiyo mbaya.
Familia hiyo inayoishi eneo la Hayes Magharibi mwa London, iliongeza kusema: "Bolutito alikuwa mtoto wetu wa kwanza na alikuwa nuru kwetu. ''
"alikuwa mrembo, mwenye maadili mema, na mpenzi wa Ballet, na tutamkosa sana.''
Polisi walithibitisha kwamba kifo cha mtoto huyo kilikuwa ajali kwani walifika wote katika kituo cha treni na mamake, ila mtoto aligongwa na kufariki wakati mama akijaribu kuegesha gari lake.
Polisi wanachunguza tukio hilo.
via>>bbc
Social Plugin