Shy town Movement chini ya udhamini wa Modequeen wanakuletea burudani babu kubwa
kutoka kwa Mfalme wa Shinyanga (King wa Shy town) Dudu P a.k. a “Pinadda”
akizindua album yake inayoitwa “Kila Akiniona”.
Mpango mzima ni ndani ya Ukumbi wa CCM Ry-Misanga mjini
Shinyanga siku ya Jumamosi Agosti 16,2014 kuanzia Saa moja usiku hadi majogoo.
Mkali huyo atasindikizwa na wakali wengine kibao kutoka
Shinyanga akiwemo Mwakanjuki,D Mikazo,Ibra Mpanduji,R6 King Dizzo,Minad
Combination,Masha Mc,Kaizian Marley,Bad Gangster,Rama Pizzo,KC,Balalie,Mamen
Enne,Mack Fe na Big.com
Katika uzinduzi huo pia Mwana mama mkali katika miondoko
ya Taarabu Mamaa Salma Murii kutoka Shy town ataangusha bonge la burudani.
Kiingilio ni Buree!! hii ni special kwa wana wa Shinyanga.
Njoo wewe!! Yule pale!! Wale kule!! Mujionee Kazi nzuri
kutoka kwa wasanii wa Shinyanga.
Social Plugin