WATAALAMU wa masuala ya lishe wamesisitiza mtoto anapaswa kunyonyeshwa kwa dakika 45 bila kukatishwa.
Hata hivyo, imeelezwa kutokana na teknolojia za kisasa, akina mama wengi wanakiuka ushauri huo wa kitaalamu kutokana na baadhi yao kutumia muda mwingi kwa shughuli nyingine ikiwemo matumizi ya simu za mkononi.
alisema Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Augustine Massawe.
Aliyaeleza hayo juzi jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo ya waandishi wa habari katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama.
Dk Massawe aliwataka kina mama kuacha kupokea simu wakati wa kunyonyesha watoto ili kuwawezesha kunyonya ipasavyo.
Alisema matumizi ya simu ni miongoni mwa mambo yanayomvuruga mtoto wakati wa kunyonya na hasa mama anapozungumza nayo muda mrefu.
Ofisa katika Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Luitfrid Nnallu alisema tatizo la utapiamlo limeongezeka hadi kufikia asilimia 42 miongoni mwa sababu ikiwa ni ukosefu wa ujuzi wa unyonyeshaji.
Alisema tatizo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye mikoa ya Dodoma, Lindi, Rukwa na Iringa.
alisema.