MWANDISHI WA HABARI ANUSURIKA KUPIGWA NA MKUU WA POLISI WILAYA YA GEITA

Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima Wilayani Geita mkoani Geita Valence Robart amenusurika kupigwa na mkuu wa polisi wa Wilaya ya Geita,OCD Busee Bwire,muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo.

Robart alifika kituoni hapo kwa lengo la kujua maendeleo ya kesi aliyoifungua kituoni hapo Julai 23 mwaka huu baada ya kuibiwa pikipiki yake aina ya SUNLG yenye namba T 305 BWV na watu wasiojulikana.

Tukio la Mwandishi huyo kutaka kupigwa na OCD Bwire lilitokea Agosti 5 mwaka huu majira ya saa nane na nusu mchana  muda mfupi baada ya kuwasili kituoni hapo kuonana na mpelelezi wa kesi aliyoifungua dhidi ya wezi wa pikipiki yake.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza baada ya kufika kituoni hapo akiwa anazungumza na mkuu wa kituo cha polisi Geita  Enock Rayi eneo la CRO,alitokea mkuu huyo wa polisi ambaye kwa wakati huo alikuwa ofisini kwake.

‘’Unashida gani kituoni hapa?umefuata nini?OCD Bwire alimhoji mwandishi huyo na kujibiwa alichofuata ni kujua maendeleo ya jarada lake la wizi wa pikipiki yake.

Hata hivyo katika hali ambayo haikutarajiwa,OCD huyo alimtaka mwandishi huyo kuondoka mara moja eneo la kituo hicho kabla hajamtia adabu ikiwa ni pamoja na kumweka rockup.

‘’Ondoka hapa mara moja kabla sijakuweka sero,nitolee sura yako hapa mara moja’’alisikika OCD huyo akimfokea mwandishi huyo ambaye kwa hofu ya kupigwa na kuwekwa ndani alitii na kutokomea kusikojulikana.

Mwandishi huyo mapema mwezi uliopita aliibiwa pikipiki nyumbani kwake majira ya usiku wakati akiwa amelala na baadaye alitoa taarifa katika kituo cha polisi wilaya ya Geita iliyofunguliwa GE/RB/4617/2014 na jeshi hilo liliahidi kuwasaka na kuwapata.

Kitendo cha OCD Bwire kumtimua mwandishi huyo kituoni hapo ili hali alikuwa ameitwa kwenda kuonana na mpelelezi wa kesi yake kimelaaniwa na baadhi ya askari pamoja na wananchi walioshuhudia sakata hilo na kumtaka mkuu wa polisi nchini IGP Ernest Mangu kumwajibisha OCD huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni amefanya matukio ya kulidhalilisha jeshi hilo.

Tukio la kwanza ni la kuangusha gari alilokuwa akiliendesha yeye wakati likitokea katika kituo kidogo cha Nyarugusu walikofuata watuhumiwa ambao walitoroka baada ya ajali hiyo.

Tukio jingine ni la kumshambulia mkewe Taus Mashaka kwa kumpiga ngumi na mateke kisha kumuuma mdomo hali ambayo imepelekea mwanamke huyo ambaye pia ni askari polisi mwenye cheo cha meja kitengo cha usalama barabarani kutimkia nyumbani kwao Singida.

Na mwandishi wa Malunde1 blog -Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post