Wataalamu wanaokabiliana na maambukizi ya Ebola |
Serikali ya Liberia imetaka miili yote ya watu waliopoteza maisha kutokana na Virusi vya Ebola kuchomwa moto.
Waziri wa Habari Lewis Brown pia ameonya kuwa biashara zisizo na vifaa vya kunawia mikono zifungwe
Mwaka huu ugonjwa wa Ebola umegharimu maisha ya watu 728 kutoka Guinea, Liberia, Sierra Leone, ugonjwa unaoelezwa kuwa hatari zaidi.Uamuzi huo unakuja kutokana na hatua ya jamii kadhaa kuruhusu miili ya Waliopoteza maisha kuzikwa kwenye makazi yao.
Virusi vya ugonjwa huu husambaa kwa njia ya damu na majimaji kwa njia ya kugusa mwili wa mtu aliyekufa kutokana na Ebola.
Mwandishi wa BBC aliye mjini Monrovia, amesema kuwa kuchoma moto mwili si utamaduni wa Liberia na wataalam wa afya wanasema shughulli za mazishi pia zimesababisha kusambaa kwa virusi.
katika hatua nyingine, Marekani ina mpango wa kutuma wataalam wake wa afya takriban 50 katika kipindi cha siku 30 zijazo kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ebola.
Inaelezwa kuwa hakuna dawa wala kinga ya ebola isipokuwa mgonjwa hupona ikiwa atapatiwa matibabu mapema.
Hivi sasa ugonjwa huu unaua kati ya 50% na 60% ya walioathirika.
Social Plugin