Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog,picha ikimwonesha mwanamke akiwa katika mashindano ya mbio za baiskeli huku akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani.Kesho katika uwanja wa ccm Kambarage mjini Shinyanga katika kusherehekea sikukuu ya Nane nane mbio za namna hiyo zitakuwepo
Mashindano
ya mbio za baiskeli kwa kanda ya ziwa na mashariki yanayojulikana kama
(safari lager bike race 2014) yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa mjini Shinyanga kwa ikiwa ni ngazi ya mkoa katika uwanja wa CCM Kambarage wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima
nchini (Nane Nane).
Kwa
mujibu wa meneja mauzo wa TBL kanda ya magharibi Robert Kazinza lengo kuu la
mashindano hayo ni kujenga uhusiano wa kimichezo kupitia mchezo wa
Baiskeli,kupromote bia safari lager kupitia kampuni ya TBL,kutoa burudani,kusapoti sera ya
serikali ya kuinua michezo.
Amesema mashindano hayo katika miaka yote yamekuwa yakidhaminiwa
na TBL kupitia bia yake ya Safar Lager na kwa ngazi ya mkoa mwaka huu
yanafanyika mkoani Shinyanga na kikanda yatafanyika jijini Mwanza.
Kazinza amesema
lengo la kampuni ya TBL kupitia bia ya safari lager kudhamini mashindano hayo
ni kufufua mitaji ya wajasiliamali kanda ya ziwa kwa kuwa michezo ni ajira.
Tayari washiriki wameshawasili
tayari mjini Shinyanga kwa ajili ya mashindano hayo kuanzia saa moja asubuhi
ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Amesema zawadi
za mashindano hayo kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume(Mbio za baiskeli
kutoka uwanja wa Kambarage-Kahama/Kahama-Shinyanga) ambapo ni sawa na kilomita
250 ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja, mshindi wa pili shilingi
laki nane na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki sita,mshindi wa nne
laki 5,mshindi wa tano laki 3,mshindi wa 6 hadi kumi ataondoka na shilingi laki
moja,na mshindi wa 11 hadi 20 watapata shilingi elfu 50.
Kazinza ameongeza kuwa mshindi wa
kwanza kwa mbio za wanawake kilomita 150(Shinyanga-Isaka/Isaka-Shinyanga)
atajizolea kiasi cha shilingi laki saba, mshindi wa pili laki tano na mshindi
wa tatu atajibebea kiasi cha shilingi laki tatu, wa laki 2, wa tano laki moja
na nusu,wa sita hado wa 10 ataondoka na shilingi laki , na mshindi wa 11 hadi 20 ataondoka na
shilingi elfu 50 kila mmoja.
Pia kutakuwepo mbio za watu wenye ulemavu pamoja mbio za akinamama wakiwa
wamebeba ndoo za maji kichwani kuzunguka uwanja wa Kambarage ambapo
washindi wote watapatiwa zawadi nono.
Katika kunogesha sikukuu ya wakulima pia kutakuwepo na ngoma za asili na shamra shamra
zitaanza saa mbili asubuhi katika uwanja wa Kambarage.
Mashindano
ya mbio za baiskeli kwa kanda ya ziwa na mashariki yanayojulikana kama
(safari lager bike race 2014) yalianza rasmi mwaka 1998, na yalianzia mkoani Mwanza na mwaka huu ni awamu ya 16 tangu kuanza kwake.
Social Plugin