Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA_SHIRIKA LA EGPAF LAANZA ZIARA MKOANI SHINYANGA


Ziara ilianzia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ndugu Mohammed Kiyungi(kulia) Agosti 12,2014.Ni ziara ya mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) bi Mercy Nyanda(Kushoto) kutoka Dar es salaam.Shirika la EGPAF linajihusisha suala la kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto likifadhiliwa na msaada wa watu wa Marekani kupitia Shirika la USAID na CDC.Ziara hiyo ya siku 4 mkoani Shinyanga inalenga kutathmini utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na EGPAF kama vile kuhusu Uzazi wa mpango na uchunguzi kuhusu Shingo ya Kizazi

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ndugu Mohammed Kiyungi akizungumza na mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) bi Mercy Nyanda pamoja na waandishi wa habari waliokuwa wameambatana na mratibu huyo katika ziara hiyo.Pamoja na mambo mengine Kiyungi alisema hivi sasa katika wilaya yake hali ya utoaji huduma ya afya ni nzuri ukilinganisha na siku zilizopita huku akilipongeza shirika la EGPAF chini ya ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Shirika la USAID na CDC kwa kazi nzuri kwani limekuwa mstari wa mbele katika kusaidia/jamii katika sekta ya afya katika wilaya hiyo katika kuhamasisha uzazi wa mpango na kupiga vita saratani ya shingo ya kizazi

Ziara inaendelea_Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dr Archie Hellar akizungumza na mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF bi Mercy Nyanda na waandishi wa habari.Dr Hellar alisema EGPAF kupitia programu zake kuhusu uchunguzi wa kansa ya saratani ya shingo ya kizazi katika Kituo cha afya cha Nindo pamoja na programu ya uzazi wa mpango katika vituo vyote 35 vya afya katika wilaya hiyo.Alisema EGPAF ikifadhiliwa na  watu wa Marekani kupitia Shirika la USAID na CDC wamekuwa wakisaidia kuwajengea uwezo wataalam wa afya,kusambaza vifaa kwa ajili ya tiba.

Mratibu wa afya ya uzazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Esteria Gutenga akielezea juu ya uchunguzi kuhusu shingo ya kizazi na jinsi utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango pamoja na mikakati mbalimbali katika kukabiliana na changamoto ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwa mtoto katika wilaya hiyo.Gutenga alitumia fursa hiyo kuwataka akina mama kunyonyesha watoto wao miezi 6 bila kuwapa chakula kingine 

Ziara inaendelea_Hapa ni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga,katika kitengo cha  Uzazi wa Mpango-Pichani ni afisa muuguzi katika hospitali hiyo Maria Rose Barikwingenza akizungumzia kuhusu uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi katika hospitali hiyo.Alisema yeye ni miongoni mwa wataalam waliojengewa uwezo na shirika la EGPAF lililofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la USAID na CDC,walianza mwaka 2013 na akina mama wengi hususani kutoka manispaa ya Shinyanga wamekuwa wakijitokeza kupima afya zao

Waandishi wa habari wakiandika mawili matatu kutoka kwa mtaalam wa afya
Kulia ni muuguzi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth Sabuni ambaye pia alipatiwa mafunzo na shirika la EGPAF kuhusu Uzazi wa mpango akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu uzazi wa mpango kwa wanandoa na wasio wanandoa.Aliwataka wazazi na walezi kuzungumza na watoto wao kuhusu uzazi wa mpango ili kuepuka mimba za utotoni,huku akiwasisitiza akina mama kutumia njia ya kitanzi kupanga uzazi pamoja na kwamba wengi wanatumia sindano katika kupanga uzazi

Afisa muuguzi katika hospitali hiyo Maria Rose Barikwingenza akionesha kifaa kinachotumika kutibu saratini ya shingo ya kizazi,miongoni ,mwa vifaa vilivyotolewa na shirika la  EGPAF lililofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la USAID na CDC

Wauguzi waliojengewa uwezo na shirika la EGPAF wakiwaonesha waandishi wa habari vifaa wanavyotumia katika kitengo cha uzazi wa mpango katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga

Kushoto ni mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) bi Mercy Nyanda akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa muuguzi katika hospitali hiyo Maria Rose Barikwingenza 
Wa tatu kutoka kushoto ni nesi kiongozi wodi za wazazi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga Fatuma Bwanga akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari baada ya kuingia katika wodi ya wazazi ili kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu uzazi wa mpango.Waandishi hao wa habari walikuwa wameambatana na mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) bi Mercy Nyanda
Ndani ya wodi ya wazazi_Mmoja wa wazazi ambaye amejifungua katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga akimnyonyesha mtoto wake na kueleza kufurahishwa na namna anavyopanga uzazi na mme wake katika kuhakikisha kuwa mtoto anakuwa na afya nzuri
Kushoto ni mtaribu wa kitengo cha Mawasiliano na Utetezi kutoka shirika la EGPAF(Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation) bi Mercy Nyanda akiwa amembeba mtoto  Dotto,ambaye ni mtoto wa bi Neema Lucas(kulia) aliyejifungua watoto mapacha katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
Hapa ni ndani ya moja ya wodi za wazazi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga,wodi za hospitali ya mkoa wa Shinyanga ni safi kama unavyoona pichani.Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com