|
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino)wasioona na wasiosikia cha Buhangija mjini Shinyanga ambapo leo Mjasiriamali(mfanyabiashara) kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam,ambaye asili yake ni mkoa wa Shinyanga(Matanda) bi Mwashi Kija Silasi amefika katika kituo hicho na kutoa msaada wa nguo zikiwemo suruali,mashuka mashati,na miamvuli pamoja na vitu vingine kama vile mchele,mkaa,mafuta maalum ya kujipaka kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi,sukari,maharage,sabuni,mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.
Mbali na kutoa zawadi hizo watoto hao ambao sasa wako 270 pia wamekula chakula cha mchana na mjasiriamali huyo aliyekuwa ameambatana na familia yake.Pichani hapo juu ni nguo kwa ajili ya watoto hao-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mpango mzima ulianzia kwenye Chakula cha Pamoja_Watoto wakinawa tayari kabisa kula chakula kilichoandaliwa na mjasiriamali kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam Mwashi Kija Silasi ambaye alipata taarifa kuhusu kituo cha Buhangija kupitia mtandao huu wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga na kuguswa na hali ya maisha magumu wanayoishi watoto hao na kuamua kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Shinyanga,msaada aliotoa leo ni wa kwake kwa kushirikiana na rafiki zake wa karibu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Aliyeshikilia sahani ya chakula upande wa kulia ni mjasiriamali kutoka Dar es salaam,bi Mwashi Kija Silasi akichukua chakula kwa ajili ya kuwapatia watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija mchana wa leo kituoni hapo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Zoezi la ugawaji chakula likiendelea_Wa tatu kutoka kushoto ni bi Mwashi Kija Silasi akishirikiana na mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu kituo cha Buhangija mjini Shinyanga bi Maisara Adinan kugawa chakula kwa watoto leo mchana,wa kwanza kushoto ni mmoja wa wanafamilia ya bi Mwashi walioambatana naye katika kituo hicho akisaidia kugawa chakula-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Watoto wanakula chakula kwa uangalizi wa karibu kabisa kutoka kwa walimu walezi wa watoto hao ambapo hivi sasa wenye ulemavu wa ngozi wako 178,wasioona 40 na wasiosikia 52-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Chakula kilikuwepo cha kutosha,nyama kwa sana,wali kama kawaida,pilau ya kutosha,watu wote walikula na kusaza-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Baada ya chakula_Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija ambaye pia ni mlezi mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi bwana Peter Ajali akimkaribisha bi Mwashi aliyepeleka msaada leo wa chakula na mavazi katika kituo hicho ambapo pamoja na mambo mengine alimpongeza mjasiriamali huyo kwa kuwa na moyo wa upendo kwa watoto hao na kuitaka jamii kuiga mfano wake kwani ameshangaa kuona akisafiri kutoka Dar es salaam kwa ajili ya watoto wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Katikati ni mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam bi Mwashi Kija Silasi akizungumza katika kituo hicho ambapo alisema aliguswa na maisha wanayoishi watoto hao hivyo kuamua kuandaa chakula cha pamoja na zawadi zingine kwa watoto hao zaidi ya 200.Alitaja vitu alivyoleta kuwa ni nguo yakiwemo mashuka,mashati na suruali,miamvuli,mafuta ya kujipaka na kupikia,mchele,sukari,dagaa kwa wenye mahitaji maalum,mkaa,maharage vyote vikiwa na thamani ya mamilioni ya fedha yote hiyo ni kwa sababu ya upendo kwa watoto hao.Nyuma yake ni marobota ya nguo alizokuja nazo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam mwenyeji wa Shinyanga bi Mwashi Kija Silasi akizungumza na watoto hao ambapo aliwataka,kusoma kwa bidii kupendana,wasigombane na kujimbua na kujiamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa katika nchi hii kwani hawana utofauti na watu wengine isipokuwa ngozi tu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Wa pili kutoka kushoto ni Mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam bi Mwashi Kija Silasi akikabidhi Mwamvuli kwa mtoto Kabula Nkarango kutoka Kahama ambaye mwaka 2010 alikatwa mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nao kusikojulikana.Jumla ya miamvuli 150 imekabidhiwa kwa watoto wenye ulemavu hususani wale wakubwa kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya jua wanapotembea-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Watoto wakifurahia miamvuli yao baada ya kukabidhiwa leo mchana-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Kila mtoto alipata shuka yake,pichani watoto wakiangalia shuka walizopewa leo na mjasiriamali kutoka Dar es salaam ambaye alipata taarifa kuhusu kuwepo kwa kituo cha Buhangija kupitia mtandao huu wa Malunde1 blog-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Kulia ni Mlezi mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwa ameshikilia nguo kwa ajili ya watoto wa kiume mashati na suruali zilizoletwa na Mwanamama Mwashi kutoka Dar es salaam(kushoto kwake)-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam bi Mwashi Kija Silasi akikabidhi sabuni za kufulia kwa watoto hao leo mchana-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mtoto Kabula Nkarango ambaye alikatwa mkono wake na watu wabaya huko Kahama.Hapa ameshikilia mafuta,sabuni,mwavuli na soda yake vyote vikiwa vimeletwa na mwanamama Mwashi,mwenyeji wa Shinyanga lakini kikazi maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Picha ya pamoja_Mfanyabiashara Mwashi Kija Silasi,akiwa na familia yake na watoto wenye ulemavu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu leo kituoni hapo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mwalimu Peter Ajali akitoa neno la shukrani baada ya zoezi la kukabidhi msaada kuisha-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Watoto wakibembea baada ya kula,kupokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara Mwashi Kija Silasi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin