Ukistajabu ya Mussa, utapata ya Firauni,mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu (jina linahifadhiwa),mkazi wa Sokoni One jijini Arusha, amebakwa na kunajisiwa na mwanamme mwenye umri wa miaka 30.
Mtuhumiwa ametajwa kwa jina la Rajabu Mkoba, mkazi wa eneo hilo.
Ilidaiwa mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo kwa zaidi ya saa 9 baada ya kumchukua kwa mtu aliepewa kumtunza.
Tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu huku mama mzazi wa mtoto huyo, Mwitango Yambazi Mtalu (27), akishindwa kutoa taarifa polisi baada ya kuahidiwa shilingi 100,000.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mama wa mtoto huyo, alisema siku ya Jumapili majira ya asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga, ili apate nafasi ya kushiriki mkutano wa kikundi chake.
Na Joseph Ngilisho-Arusha
Social Plugin