Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari
Shinyanga Dickson Jones(17)amefariki dunia
baada ya gari alilokuwa anasafiria na wenzake kupinduka katika barabara ya
Shinyanga kuelekea Maswa katika kijiji na kata ya Mwigumbi wilayani Kishapu
mkoani Shinyanga kutokana na kile kilidaiwa kuwa mwendo kasi.
Kamanda Kamugisha amesema tukio hilo limetokea janasaa moja usiku ambapo gari lenye namba za usajili T116 BDF aina ya
Toyota mali ya Washi Construction ya Geita likiendeshwa na dereva asiyejulikana
jina wala makazi yake likitoka Maswa kwenda Shinyanga lilipinduka na kusababisha
kifo cha mwanafunzi huyo papo hapo.
Amewataja majeruhi kuwa ni Kefa Japhet(20)ambaye
ameuamia mguu wa kushoto na Hosea Japhet(18)aliyeumia mgongo, wote wanafunzi wa
kidato cha tatu katika shule ya sekondari Shinyanga na Ramadhani
Mazuri(23) mkazi wa Kahama aliyeumia mkono na mguu wa kushoto na
wamelazwa katika hospitali ya
mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin