Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YULE MWANAMUZIKI ALIYEKATA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KISA MWANAMKE AFUNGUKA,ASEMA ALICHOKIKATA NDIYO "CHANZO CHA MATATIZO"

 


Je unamkumbuka mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson ambaye alikata Uume wake mwezi Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya hivyo..

Johnson, aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili. 

 
Madaktari walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake.

Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua wiki hii kujieleza kwa nini alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha televisheni cha E! nchini Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya , lakini nilikuwa najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'

Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu. Suluhu langu kwa masahibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, 'mimi ni mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi. Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''

Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio kichaa.
 
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo. 

''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu. ''

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com