Habari Mpya

    Loading......

AJALI TENA _ GARI LA JESHI LA WANANCHI TANZANIA LAPATA AJALI ASUBUHI HII,YADAIWA WATATU WAMEKUFA

Kutoka Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga kuhusu ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la Wananchi Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo na shuhuda wa eneo hilo.

Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo ya Mnolela kijijini Lindi.

kwa mujibu wa shuhuda amesema gari/kifaru kimeparamia nyumba ya mtu na kuua wanajeshi 3 na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke aliyekua kalala ndani.
Madhara mengine yaliyotokana na ajali hii ni nyumba mbili kuharibika vibaya,majeruhi wa ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara.

via>TZA
TUNAPENDA TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA, LIKE PAGE YETU SASA HIVI UENDE NA WAKATI. BONYEZA HAYA MANENO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com