Kara Lee akimlisha keki mumewe Richard Miller mara baada ya kufunga ndoa katika Mlima Kilimanjaro juzi
Kara Lee akimvisha pete mumewe Richard Miller
Kara Lee anasimulia hivi: “Katika Sikukuu ya Krismas huko Minnesota nchini Marekani tulivishana pete mimi na mchumba wangu Richard Miller na kuwekeana ahadi kuwa ndoa yetu lazima ifungwe juu ya paa la Afrika na hiyo sehemu si nyingine zaidi ya Mlima Kilimanjaro”.
Wanandoa hao wakisaini kitabu cha maharusi
Safari yao ya kupanda mlima huo ilikuwa ikiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Zara iliyopo mjini Moshi, Kilimanjaro ambapo Septemba 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wawili hao waliwasili katika pango la Shira wakitokea banda la Machame wakiwa pamoja na wenyeji wao tayari kwa ndoa yao hiyo iliyokuwa gumzo kwa watu waliohudhuria.
Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha akiwafungisha ndoa Kara na Richard.
Maharusi hao wakisimamiwa na Ansigar Mtandika na Neema Njau, walianza kula viapo vya ndoa pamoja na kuvishana pete mbele ya mchungaji huyo huku wakiahidi kuwa pamoja katika shida na raha mpaka
Mwenyezi Mungu atakapowachukua.
Wanandoa hao katika pozi baada ya kufunga ndoa.
Richard na Kara walianza maisha ya mke na mume katika hema na leo wameendelea na safari yao ya kuupanda mpaka kileleni Mlima Kilimanjaro ambapo wamefika kituo cha Baranco. Wanandoa hao
wanataraji kufika kilele cha mlima huo kesho Jumatano na wataanza kushuka kuelekea geti la Mweka Keshokutwa Alhamisi ya Septemba 25, 2014.
“Wana nguvu na wamepania kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na naamini watatimiza ndoto yao nyingine hiyo," alisema Teophil Karia, mwongoza wageni kutoka Zara Tours.
BONYEZA HAYA MANENO TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA