Aliyesimama ni mkuu wa kitengo cha sheria kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya African Barrick Gold bi Katrine White kutoka London ,nchini Uingereza ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi ya ufadhili katika mradi wa Can Educate akizungumza katika hafla maalum ya kuwapongeza wahitimu kidato cha 6 mwaka 2014 katika shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo katika halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga.
Hafla hiyo maalum imeandaliwa na ABG-Buzwagi baada ya kufurahishwa na matokeo ya wanafunzi 15 waliowafadhili wote kupata daraja la kwanza.Katrine White alisema mradi wa Can Educate umeanza mwaka 2013 ukihusisha wanafunzi shule za sekondari na wanawalipia ada,sare na vifaa vingine muhimu vya shule.Bi White aliwataka wanafunzi wanaonufaika na mradi huo wawe mfano mzuri kama wenzao waliomaliza masomo yao mwaka huu kwa kufanya vizuri katika mtihani wao wa kidato cha 6
|
Ndani ya ukumbi wa shule ya sekondari Mwendakulima ambapo leo African Barrick Gold imefanya hafla maalum kuwapongeza wanafunzi 15 kutoka shule hiyo waliomaliza kidato cha sita mwaka 2014 kwa kufanya vizuri katika mtihani wao wa mwisho.Jumla ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita ni 23 kati yao 15 waliopata daraja la kwanza walikuwa wanasomeshwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold kupitia mgodi wake wa Buzwagi kupitia mradi wake wa Can Educate unao waolenga zaidi watoto kutoka familia zenye kipato duni,yatima na wale wanaojitahidi katika masomo yao ambapo mgodi umekuwa ukiwalipia ada,kuwapa sare na vifaa muhimu vya shule.
Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Katrine White kutoka London nchini Uingereza ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi ya ufadhili katika mradi wa Can Educate
Aliyesimama ni meneja wa mgodi wa Buzwagi bwana Philbert Rweyemamu akizungumza leo katika shule ya sekondari Mwendakulima.Alisema ABG ina kila sababu ya kuwapongeza wanafunzi hao 15 na kuwapa jina la "Mashujaa" na kwamba wanafunzi hao ni matunda ya mgodi huku akiitaka jamii kuacha kubeza shule za kata.
Wanafunzi wanaosoma kidato cha sita mwaka 2014 katika shule ya sekondari Mwendakulima wamsikiliza kwa makini meneja wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu aliyewataka kujibibidisha katika masomo na kufuata nyayo za dada zao walioonesha mfano wa kuigwa
Rweyemamu alisema matokeo mazuri ya wanafunzi hao yanawapa moyo kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu.Aliongeza kuwa kupitia mradi wa Can Educate mwaka huu zimetengwa dola laki 1 na kwamba zaidi ya wanafunzi 400 katika halmashauri ya mji Kahama wanafadhiliwa na African Barrick Gold .Pichani kulia kwake ni mgeni rasmi katika hafla hiyo ,mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Katrine White kutoka London Uingereza ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi ya ufadhili katika mradi wa Can Educate
Aliyesimama ni mkuu wa shule ya sekondari Mwendakulima bi Dianal Kuboja akizungumza wakati wa hafla hiyo maalum iliyoandaliwa na ABG-Buzwagi ambapo alisema katika matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 mwaka huu shule yake ya kata imekuwa ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga na ya 9 kitaifa kati ya shule 180 zenye wanafunzi wachache na imeongoza katika kanda ya magharibi.
Alisema kati ya wanafunzi wote 23,15 walikuwa wanafadhiliwa na ABG-Buzwagi na wote wamepata daraja la kwanza na 8 waliobaki wote walipata daraja la pili.Hata hivyo aliupongeza mgodi huo kwa kuwa karibu na wananchi wanaowazunguka na kuwataka kuendelea kusaidia katika sekta ya elimu na kuwafikia wanafunzi wengi zaidi kutoka familia zenye kipato duni.Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Catrine White kutoka London Uingereza( wa pili kutoka kulia pichani) |
|
Pichani ambao hawajavaa sare za shule ni wawakilishi watano wa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita katika shule ya Mwendakulima,wengine ni wanafunzi kidato cha 4,5 na 6 mwaka huu wakiwa ukumbi wa shule hiyo wakati wa hafla maalum kuwapongeza wahitimu kidato cha 6 mwaka huu waliofanya vyema katika mtihani wao
Aliyesimama ni mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mwendakulima bi Anna Magesa akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo aliwataka wanafunzi wanaofadhiliwa na mgodi kutumia fursa hiyo vizuri ili kuendelea kuwapa moyo ABG Buzwagi kwani wanatoa fedha nyingi kusaidia wanafunzi hao |
Walimu katika shule ya sekondari Mwendakulima wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini leo
|
Wanafunzi katika shule ya sekondari Mwendakulima wakifuatilia kwa ukaribu zaidi kilichokuwa kinajiri ukumbini leo.Wanafunzi hao waliaswa kutumia fursa ya mgodi wa Buzwagi kujitahidi katika masomo yao. |
|
Aliyesimama ni afisa elimu taaluma sekondari halmashauri ya mji Kahama bwana Richard Msagati,ambaye alimwakilisha mkurugenzi wa halmashauri hiyo akizungumza wakati wa hafla hiyo.Pamoja na kuipongeza kampuni ya African Barrick Gold kusaidia katika sekta ya elimu kwa kuwapa ada,sare za shule na vifaa vingine vya shule pia aliwataka kusoma kwa ushindani wa kitaifa ili kuipa shule,wilaya na mkoa kwa ujumla heshima.
"Leo tupo hapa kwa sababu ya matokeo mazuri,matokeo haya yanafany shule yenu iheshimike katika jamii,nimeambiwa sasa hivi kila mzazi anataka mtoto wake aje kusoma hapa",aliongeza |
Tukio hilo la aina yake lilikuwa kivutio kwa yeyote mwenye mapenzi mema na sekta ya elimu hapa nchini.
Mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Katrine White akijiandaa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha 6 mwaka 2014 shule ya sekondari Mwendakulima waliofanya vyema katika mtihani wao wa mwisho
|
Katika tukio hilo wahitimu 15 "Mashujaa"kidato cha sita 2014 walipewa vyeti na African Barrick Gold- Wa tatu kutoka kulia ni mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Katrine White akikabidhi cheti kwa Veronica Samson
|
Veronica Sayu akipokea cheti na kushikana mkono na mgeni rasmi Katrine White kutoka ABG
Mmoja kati ya wahitimu 15 kidato cha 6 shule ya kata ya Mwendakulima waliopta daraja la kwanza mwaka 2014,Mary Joseph akipokea cheti
|
Kushoto ni afisa mawasiliano ABG-Buzwagi bi Blandina Munghezi,kulia kwake ni afisa uhusiano ABG-Buzwagi bwana Moses Msofe,akifuatiwa na meneja uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanza |
Mmoja kati ya wahitimu 15 waliokuwa wanafadhiliwa na African Barrick Gold,Theleza Maziku akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake.Pamoja na kueleza furaha yake na kuishukuru kampuni ya ABG na walimu wao, pia aliiomba ABG kuendelea kusaidia wanafunzi ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya elimu katika jamii
|
African Barrick Gold pia walitoa zawadi kwa walimu wa shule ya sekondari Mwendakulima-Pichani ni mwalimu Sonda akionesha kikombe cha maajabu"Magic cup" alichopewa kama zawadi.Kikombe hicho kina rangi ya Bluu,lakini ukiweka maji/kimiminika cha moto kinabadili rangi na kuwa cheupe na kuonesha maneno "Buzwagi Gold Mine,Congratulates thr class of 2014 Mwendakulima High School",lakini ukiweka maji/kimiminika cha baridi kinabadilika rangi na kuwa cha bluu. |
|
Wa pili kushoto ni afisa mahusiano ABG-Buzwagi bi Dorothy Bikurakule akionesha maajabu ya vikombe walivyopewa walimu wanaofundisha katika shule ya sekondari Mwendakulima |
|
Moja ya kikombe baada ya kuwekewa maji ya moto kikabadili rangi kutoa bluu na kuwa cheupe |
|
Waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Picha ya pamoja wahitimu watano kati ya 15 waliokuwa wanafadhiliwa na ABG wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu
|
Walimu ,wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu |
|
Picha ya pamoja-viongozi wa ABG,wahitimu,walimu |
Mkuu wa shule ya sekondari Mwendakulima bi Dianal Kuboja akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla hiyo maalum ambapo aliwataka wadau mbalimbali sekta ya elimu kusaidia sekta hiyo hususani katika suala la chakula na malazi kwa wanafunzi
Nje ya ukumbi mkuu wa kitengo cha sheria ABG bi Katrine White akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema wataendelea kutoa msaada kupitia mradi wao wa CAN EDUCATE
Nje ya ukumbi-baadhi ya wahitimu kidato cha 6,shule ya sekondari Mwendakulima waliopata daraja la kwanza wakibadilishana mawazo.Wa kwanza kulia ni Mary Joseph,akifuatiwa na Theleza Maziku,Rahel Mtwale na Veronica Sayu
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com