Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News!! MTOTO AUAWA KWA KUNYONGWA KISHA KUTUPIWA KWENYE KARO LA MAJI AKICHUNGA MBUZI SHINYANGA

Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 9 ameuawa kwa kunyongwa na mwanamme ambaye hakujulikana jina wala makazi yake.

Mtoto huyo amejulikana kwa jina la Jackson mtoto wa mzee Lyimo.


Inaelezwa kuwa  mtoto huyo alipotea tangu jana wakati akichunga mbuzi na wenzake,na hakuonekana hadi usiku huu majira ya saa moja alipokutwa ameuawa na kutupiwa kwenye karo la maji machafu yanayotoka kiwanda cha Jambo kilichopo katika kata ya 
 Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia malunde1 blog kuwa mtoto huyo alikuwa anachunga mbuzi ndipo akatokea mwanamme huyo na kumnyonga shingo.


Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya mtoto Happiness Kashinje mwenye umri wa miaka 9 kuuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika katika manispaa ya Shinyanga.

Malunde1 blog inaendelea kufuatilia tukio hili,tutakuletea taarifa kamili hivi punde.......
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com