EGPAF YAKABIDHI MASHINE NA VIFAA TIBA KUTIBU DALILI ZA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOANI LINDI

Hapa ni katika hospitali ya wilaya ya Kinyonga- Kilwa mkoani Lindi ambapo jana Septemba 24,2014 ambapo EGPAF imekabidhi mashine za  "cryotherapy" pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa  chini ya ufadhili wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Elizabeth  Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF)Tanzania, kupitia shirika la Centre for Disease Control and Prevention (CDC) lililopo chini ya serikali ya Marekani.

Mashine hizo zimekabidhiwa katika mkoa wa Lindi hospitali ya mkoa Sokoine, hospitali ya wilaya ya Kinyonga- Kilwa na hospitali ya wilaya ya Nachingwea – Nachingwea.

Pichani (kushoto) ni m
ratibu wa afya ya uzazi na jinsia kutoka EGPAF, Angesyege Kibona akitoa maelezo kuhusu mashine hiyo ya cryotherapy kwa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilwa ndugu Abdallah Ulega.Mashine hizo zitatumika katika kutibu dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake  wa mkoa wa Lindi.
 
 Katikati ni meneja mradi wa huduma za matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU kutoka EGPAF, Dkt Juma Somgoro akitoa maelezo ya nyongeza kuhusu mashine hiyo ya cryotherapy jinsi inavyoweza kutibu dalili za  awali za saratani ya mlango wa kizazi.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega.
 Zoezi hilo la makabidhiano kwa niaba ya mkoa wa lindi lilifanyika wilayani kilwa katika hospitali ya wilaya ya Kinyonga, na kushuhudiwa na watu mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kilwa ndugu Abdallah Ulega, Mkurugenzi wa wilaya ya Kilwa ndugu Mtanda, wauguzi wa hospitali ya kinyonga, wafanyakazi wa EGPAF na watu mbalimbali

Kushoto ni mratibu wa afya ya uzazi na jinsia kutoka EGPAF, Angesyege Kibona akikabidhi mashine ya cryotherapy kwa mkuu wa wilaya ya Kilwa ndugu Abdallah Ulega ili aikabidhi rasmi kwa hospitali ya Kinyonga - Kilwa.
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilwa nduguAbdallah Ulega akabidhi rasmi mashine hiyo kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kinyonga- Kilwa Dkt Dominic Kitego
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akizunguma wakati zoezi la kukabidhi mashine hizo ambapo alisisitiza juu ya umuhimu wa mashine hizo katika kusaidia upatikanaji wa matibabu ya dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi hasa kwa watu wanaoishi na VVU.
Aliyesimama ni mganga mkuu wa wilaya ya Lindi, Dkt Yusuph Sonda akiishukuru EGPAF kwa kuupatia mkoa wa Lindi vifaa hivyo kwani anaamini vitakua msaada mkubwa katika kuhakikisha wanawake wengi wanafikiwa na huduma hiyo.
Wakishuhudia tukio hilo katika picha ni Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kilwa – Mama Mtanda pamoja na Mganga mkuu wa wilaya ya Kilwa Dkt Peter Nsanya(kushoto).
Dkt John Ritte, Meneja mradi mkoa wa Mtwara na Lindi kutoka EGPAF akielezea miradi ya EGPAF.Tukio la kukabidhi vifaa hivyo kila hospitali hizo 3,limeenda sambamba na utoaji wa mafunzo maalumu kwa watoa huduma ya afya kutoka hospitali ya Kinyonga, Nachingwea na Sokoine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post