Geita Bwana!! JAMAA AIBA SHILINGI MILIONI 4.8 ZA HARUSI, WANA KAMATI HASIRA MWANZO MWISHO

Wanakamati waliokuwa wanaandaa harusi ya Lameck Magaka na Mbuke Mkingawakazi wa Geita mkoani Geita  wamemtaka mhasiba  waliokuwa wamemteua kwa ajili ya kutunza pesa hizo Mayenga Malugu kurudisha kiasi cha shilingi Milioni Nne Laki Nane (4,800,000/=) alizoiba wakati wa maandalizi ya harusi hiyo.

Agizo hilo limetolewa jana na wanakamati zaidi ya 100 wakati wa kuvunja kamati  hiyo  kwenye ukumbi mmoja ulioko mjini Geita  mara baada  ya Mwenyekiti wa kamati ya vinywaji   Martine Mwanageni kumtaka  mhasibu huyo kuwasomea  matumizi ya pesa walizochanga kiasi cha milioni arobaini Laki Nane (40,800,000/= zilizotolewa kwa ajili ya Harusi Hiyo. 

Alipomaliza kusema hayo wanakamati kwa ujumla walimuunga mkono Mwenyekiti huyo ambapo Mhasibu huyo Mayenga Malugu  alianza kusoma matumizi yote lakini cha kushangaza ni kwamba kiasi cha shilingi Milioni nne laki nane (4,800,000/=) hazikujulikana zilikokwenda hivyo kumtaka mhasibu huyo kurudisha pesa hizo mara moja.

Hali pia ilikuwa tete  kwa baadhi ya wanakamati waliokuwa wanampelekea pesa bila kuandikwa majina yao ambapo siku hiyo hawakuyaona na kuanza kufoka kwa nguvu na kutaka kujua pesa zao zilikwenda wapi.
"Jamani mhasibu huyu ni mwizi pesa ni nyingi sana alizoiba anatakiwa azirudishe mara moja kwani amezoea kuiba pesa zetu ,huyu si wa kwanza anatakiwa kuwajibishwa ili liwe fundisho kwa wengine", alisema mwanakamati mmoja ambaye hakuona jina lake kwenye orodha ya waliochanga.

Pamoja na mhasibu huyo kutafuna pesa hizo wanakamati walishangazwa na kitendo cha kung’ang’ania Slip ya Tshs. Mil. 15,000,000 iliyokuwa ni zawadi kwa wana ndoa hao ambapo walitumia nguvu kumnyang’anya slip hiyo. 

Baada ya wanakamati kuanza kulalamika  na kutaka kumrushia makofi mhasibu huyo,mwenyekiti wa Harusi hiyo  Chonza  alimtaka mhasibu huyo kutojitetea bali kuwaomba msamaha mara  moja wanakamati hao kwa kupoteza pesa zao inagawa hawakurdhika na kitendo hicho na kuendelea kulalamika na kuongeza kuwa hakuna kikao chochote watakachomchagua tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post