Jambazi mmoja akiwa na bunduki na risasi 47 pamoja na sare za jeshi la wananchi ameuawa na wananchi weye hasira kali wakati akijaribu kukimbia baada ya kufanya tukio la kuvunja duka na kuiba shilingi laki 7 katika eneo la melela Mvomero mkoani Morogoro.
Kamanda Polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amemtaja mtuhumiwa amefahamika kwa majina ya Antony Msandawe mkazi Kilosa Maghubike jambazi hilo usiku lilifanya tukio la kuvunja duka ambapo alikua njiani kulekea kilosa kufanya tukio jingine.
Hata hivyo askari wa barabarani walimstukia ndipo wananchi wakasaidiana na jeshi la polisi kumkimbiza ambapo alikamatwa na kupigwa na wananchi na alifariki dunia akiwa njiani kueleka hospitali.
Social Plugin