Jeshi la polisi katika wilaya ya Geita mkoani Geita,limelazimika kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi kadhaa hewani kuwatawanya waombolezaji,wa msiba wa mtoto Amani Nyakubhaho(9)mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Geita.
Tukio hilo limetokea juzi.
Mwanafunzi huyo alipoteza maisha saa 11 jioni ya Septemba 25,mwaka huu baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji ambalo limo ndani ya hifadhi ya mgodi wa GGM kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kufuatia tukio hilo waombolezaji zaidi ya 150 wakazi wa Mtaa wa Katoma mjini Geita walifika nyumbani kwa mkuu wa wilaya Manzie Mangochie saa 11 jioni kwa lengo la kumuomba awasaidie kuuamru uongozi wa kampuni ya GGM kutoa usafiri wa kusafirisha mwili wa mwanafunzi huyo kwenda kuzikwa katika kijiji cha Bugulula.
Kutokana na tukio hilo,waombolezaji wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa huo,Emmanuel Malekela,waliandamana kwenda kwa mkuu wa wilaya na kuanza kuimba nyimbo za maombolezo”Palapanda..Litalia,Palapanda..litalia Palapanda?,Palapanda litalia Palapanda watu..wote watakuwa wamekwisha nyakulia kwenda Wapi?,Kumlaki Bwana Yesu mawinguni”
Wakati wakiimba nyimbo hizo huku wakiwa nje ya nyumba ya mkuu wa wilaya wakiwa wamekaa chini,ghafla lililotokea gari la polisi likiwa na Askari zaidi ya 20 wakiwa na silaha mbalimbali zikiwemo SMG wakiongozwa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Geita(OC-CID),John Marrow na kuwaamru waombolezaji hao kuondoka eneo hilo.
Kabla hajamaliza kuongea askari hao waliwatisha kwa kuwaelekezea bunduki,huku wakiwataka watawanyike kabla ya kuanza kuwafyatua risahi hewani pamoja na mabomu ya machozi na kusababisha wananchi hao kukimbia ovyo na kungukiana huku baadhi yao wkikaamatwa akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo pamoja na mama mzazi wa marehemu,Nyamvula Nyakubhaho.
Askari walilazimika kuwashushia kipigo kikali waombolezaji hao ambao baadhi yao walikuwa wameng'ang'ania kwenye mlingoti wa bendera ya taifa na kuwatia nguvuni.
Wakati huo huo baadhi ya waandishi wawili waliofika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasikiliza malalamiko ya wananchi hao walinyang'anywa kamera zao huku nao wakiamuliwa kuondoka katika eneo hilo kwa kutishiwa kupigwa mabomu.
"Ondokeni hapa haraka mmekuja kufanya nini nitawakamata sasa hivi na kuwaweka ndani sitaki kuwaona hapa, nitavunja kamera hizi, ndizo zinazowapa kiburi na kwanini mnipige picha? alihoji John Marrow
Hata hivyo habari zinasema kuwa vurugu hizo zilitokea mara ya pili siku moja kabla baada ya wananchi hao kuzuia Greda la Mgodi kufukia dimbwi lililosababisha kifo cha mtoto huo ili kuficha ushahidi wa tukio hilo.
Baada ya kutokea tukio hilo askari walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa mtoto huyo na kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Aidha baba mzazi wa mtoto huyo,Williamu Nyakubhaho alisema mwanaye aliondoka nyumbani majira ya mchana na kwenda kusikojulikana hadi ilipofika saa 11 jioni alipoletewa taarifa za kuzama kwake katika dimbwi hilo na mtoto wa jirani yake.
Mkuu wa wilaya ya Geita,alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alisema kuwa yeye ausiki na wananchi wanatakiwa kuwa walinzi kwa watoto wao kuliko kukaa wanalalamikia yeye.
Kwa upande wake Afisa habari wa mgodi wa GGM Tenga Tenga alisema kuwa wamemtuma mwakilishi wao kwenda kuwakilisha mgodi wao kwenye mazishi ya mtoto huyo na kuwaomba wananchi kuwa na ulinzi shirikishi wakshirikiana wa walinzi wa mgodi huo.
UNGANA NASI KWA KU LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA MOJA,BONYEZA MANENO HAYA SASA
UNGANA NASI KWA KU LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA MOJA,BONYEZA MANENO HAYA SASA
Social Plugin