Kushoto ni afisa Mawasiliano mradi wa uzazi wa mpango(Advanced Family Planning) unaogharamiwa na mfuko wa Bill & Melinda Gates Institute for Population and Reproductive Health bi Harshi Hettige kutoka nchini Marekani,kulia kwake ni mkurugenzi mkuu wa mradi huo bi Beth Fredrick kutoka Marekani wakiwa katika mkutano na wawakilishi wa vyuo vikuu mkoani Shinyanga wakijadiliana namna ya kufanikisha mradi wa uzazi wa mpango wakitumia wataalam kutoka Chuo cha Kolandoto
Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga ,ambao ni wadau wa mradi wa Uzazi wa mpango katika vyuo vikuu.Manjerenga alisema wao wanajihusisha zaidi na masuala ya vijana na hivi karibuni walifanya utafiti katika elimu ya juu na kubaini kuwa vijana wengi wamekosa elimu ya uzazi wa mpango matokeo yake wanapata maambukizi ya VVU,magonjwa ya zinaa,kupata mimba zisizotarajiwa na utoaji wa mimba kiholela hivyo wakaona umhimu wa kuwapa elimu ya uzazi wa mpango.Kulia kwake ni Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA),Moses Mongo
Majadiliano yanaendelea
Mkurugenzi mkuu wa mradi wa Uzazi wa mpango katika elimu ya vyuo vikuu bi Beth Fredrick kutoka Marekani akizungumza katika mkutano huo ambapo alipendekeza kila chuo kipange ratiba yake ili kufanikisha mradi huo ambao unalenga kusaidia vijana walioko vyuoni kwani imebainika kuwa wengi wao wanahitaji elimu ya uzazi wa mpango ili kufikia malengo yao
Mwalimu Christian Balalusesa kutoka chuo cha VETA Shinyanga akiwa ukumbini
Kushoto ni mkuu wa idara ya uuguzi chuo cha Kolandoto Dkt Paschal Shiluka akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema chuo chake akimejitolea kuwafikia wanafunzi wa elimu ya juu(vyuo vikuu) kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango ikiwa ni sehemu ya kazi ya chuo ambazo ni pamoja na kufundisha,kutoa huduma na utafiti.Dkt Shiluka alitoa wito kwa wanafunzi kujitokeza kupata elimu hiyo pindi mradi utakapoanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka huu
Afisa Mawasiliano mradi wa uzazi wa mpango(Advanced Family Planning) unaogharamiwa na mfuko wa Bill & Melinda Gates,bi Harshi Hettige akifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinajiri ukumbini leo
Kushoto ni katibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga Yusuph John |
Katika kufanikisha mradi wa uzazi wa mpango katika vyuo vikuu,PSI watashiriki katika kuhakikisha kuwa vijana wanafikiwa kwani lengo la mradi huo unajihusisha zaidi na utetezi wa mambo ya uzazi wa mpango.Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kuna huduma na uwekezaji katka uzazi wa mpango,kulinda afya ya mama na mtoto.Kupitia mradi huo vijana walioko vyuoni watapata ushauri,taarifa na huduma mbalimbali kuhusu uzazi wa mpango kutokana na mtandao wa vyuo husika kusaidiana kitaaluma.
Picha ya pamoja waliohudhiria mkutano huo |
Picha ya pamoja |
PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE-MALUNDE1 BLOG
Social Plugin