Habari zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba kesho Jumatatu Septemba 22,2014 Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Shinyanga kitafanya Maandamano ya amani kupinga Bunge maaalum la katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Maandamanao hayo yataongozwa na viongozi wa kanda wa chadema,viongozi wa mkoa na wilaya mbalimbali za mkoa wa Shinyanga yanatarajiwa kuanza saa mbili asubuhi
Kwa mujibu wa katibu wa Chadema mkoa wa Shinyanga Zacharia Thomas Obadi maandamano hayo yataanzia katika ofisi ya Chadema mkoa na kuelekea katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako watafanya mkutano wa hadhara.
Katika taarifa yake ameliomba jeshi la polisi kutoingilia kati maandamano hayo kwani ni maandamano ya amani yanayolenga kupinga matumizi mabaya ya pesa za wananchi yanayofanywa na bunge maalum la katiba.
Hata hivyo akizungumza na Malunde1 blog hivi punde kwa njia ya simu kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athumani amesema jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga halijatoa kibali kwa chama hicho kufanya maandamano hivyo kuwataka wananchi kufuata utii wa sheria bila shuruti.
Aidha amesema jeshi la polisi harijaridhia kufanyika kwa maandamano kutokana na hali iliyopo nchini na hayo ni maagizo ya jeshi la polisi nchini kwamba hivi sasa hawaruhusu maandamano kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Na Kadama Malunde-Shinyanga