Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hot News!! FREEMAN MBOWE ATANGAZWA MSHINDI MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA



Freeman Mbowe atangazwa usiku huu kuwa ndiye mshindi nafasi ya mwenyekiti Chadema uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.Ushindi wa Freeman Mbowe ni asilimia 97.3%

Sasa ni Rasmi Freeman Mbowe ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi cha tatu cha mwaka 2014-2019

PROFESA ABDALLAH SAFARI,Ndiye Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa.


*******SOMA ZAIDI HAPA UONE MAMBO YOTE YALIYOJIRI UKUMBINI LEO MWANZO HADI MWISHO*****
Igwee Bin Haki's photo.
Wageni waalikwa
Mabalozi
1. Mkuu wa EU nchini
2. Balozi wa Ubelgiji
3. Balozi wa Italy
4. Katibu wa 2 kutoka ubalozi wa Ireland hapa Tanz.
5. Balozi wa SA
6. Balozi Ubalozi wa German hapa Tz
 7. Balozi wa China hapa Tz
WENGINE
10. Wawakilishi wa Chama cha Orange wakimwakilisha Odinga
11. MKurugenzi wa idara ya njeWA cOND dENMARKJ
12. Mbunge GERMAN AKIWAKILISHA CHAMA TAWALA CDU

WAWAKILISHI WA DINI
Sheikh Katimba
Sheikh Mwangasa
Daniel Lowa

WENGINE
Jaji Mutungi-msajali wa vyama vya Siasa
Mama Mary- anamwakilisha mkurugenzi wa Takukuru

VIONGOZI MEZA KUU

1.Prof Ibrahim Lipumba-Mwy wa CUF na Mwy Mwenza wa UKAWA
2.James Mbatia-Mwy wa NCCR-MAGEUZA na Mwy mwenza UKAWA
3.E. Makaidi Mwy wa NLD
4. Philip Mangula- anamwakilisha JK, pia anamwakilisha KInana aliyeomba radhi
5. Nassoro Madhrui-Waziri SEr Mapinduzi ZNZ na naibu katibu mkuu CUF ZNZ
6. Mwatwange-Katibu mkuu wa NLD
7. Abdul Muya naibu katibu mkuu DP

 Wageni wengine waliendelea kufika.


Mwakilishi wa ODM kutoka kenya anatoa salaam Ameleta salaam kutoka Kenya. KUTOKA KWA kwa Odinga na kutoka kwa wanachama wao. 

Mwakilishi wa Conservative party -Denmark Amesema wanajivunia kusaidia Chadema kwa kutoa mafunzo
Tutasaidia wajasiriamali wadogowadogo kuona fursa, anafikiria mawazo hayo pia ni mawazo ya CDM
Anategemea ushirikiano wao na CDM utaendeelea
Sasa anampa Mwy Mbowe zawadi ya birthday yake- Mbowe alizaliwa 14 Sep miaka 53 iliyopita 

Mwakilishi kutoka CDU German
Tunapaswa kuwa na misimamo bila ya kuwa na misimamo hatuwezi kuwa na maamuzi sahihi 

John Howard aliyekuwa waziri mku wa Australia ametuma barua, iliyosomwa ya kuwatakia kila la kheri chadema, na anatazamia kuiona CDM ikiingia madarakani mwakani 

Makaidi asalimia
NLD inawaombeni mfanye mabadiliko chanya
Viongozi wenu hawa tunaimani nao tunaomba muwachague wote
NLD hasa wanawake wamenituma nitoe pongezi kubwa kwa Halima Mdee, kwamba MDEE anajua.
Baada ya kusema hayo Dunia mzima imesimama na kusikiliza maazimio ya Mkutano Mkuu, hata maadui wa CDM wanatetemeka, kwa sababu hiyo ndugu zangu wa CDM tunataka maazimio ya maana, watu wasikie, MKUTANO HUU UNATEGEMEWA PIA KUZUNGUMZA VIZURI SANA KUHUSU KATIBA YA WANANCHI.
Makaidi Akamalizia na salaam zake, Moto moto motooooooooooooooo moto moto motooooooooooooo 

salaam za Mwy wa NCCR MAGEUZI. Ndugu Mwy wa CDM, ndugu katibu Mkuu, mlezi wetu na mshauri wetu, Prof Lipumba mpambanaji mwenzetu, Comrade Mangula, Makaidi.
Ndugu zangu tunaandika historia ya Tanz, na inabidi iongozwe na viongozi makini, ili uweze kuwa kiongozi makaini lazima kuaminiana.
Sifa kuu ya kiongozi
1. Awe na uwezo wa kupanga
2. Awe na uwezo wa ku organise
3. Uwezo wa kupanga vizuri
4. Uwezo wa kusimamia
Ili Tanzania ivuke salama, tushirikiane, tuaminiane, tuvuke pamoja.
Ukishindwa kukemea onyesha hata chuki
Ninaamini wale wasiotakia mema MKUTANO HUU SASA WAMESHATULIA AHSANTENI SANA 

Mwakilishi wa Conservative party -Denmark Amesema wanajivunia kusaidia Chadema kwa kutoa mafunzo
Tutasaidia wajasiriamali wadogowadogo kuona fursa, anafikiria mawazo hayo pia ni mawazo ya CDM
Anategemea ushirikiano wao na CDM utaendeelea
Sasa anampa Mwy Mbowe zawadi ya birthday yake- Mbowe alizaliwa 14 Sep miaka 53 iliyopita



Salaam za Philip Mangula Makamu Mwy CCM Nipo hapa kwa nafasi tatu 3, 1. Makamu wa Mwy. CCM 2. Namwakilisha Rais 3. 
Sisis tunaamini siasaa sio chuki. Siasa ni tofauti ya kisera, kiitikadi kati ya kundi moja na lingine.
Tujenge utamaduni wa kukutana na kuvumiliana, tuweke maslahi ya nchi mbele.
Tuwe na political tolerance tukubali kupokea mawazo ya wengine.
Kama Yanga na Simba au waumini wa Dini mbalimbali hawanuniani, kwanini vyama vya Siasa tununiane?
Nawatakia kila la kheri katika uchaguzi wenu, uwaunganishe pamoja.
Ndugu yangu Mbowe, hongera sana na nakutakia kila la kheri, mkutano huu ni tofauti na mingine niliyowahi kuona, kuna kitu nimejifunza.
Mumevaa vizuti, lakini shari kidogo limefanana na sare zetu kichekooooo
Wajumbe wa Mkutano Mkuu oyeeeeee 




Salaam za Prof Ibrahim Lipumba Peoplessssssssssssssss, Power
Hakiiiiiiiiiiiiiiiii-SAWAAAAAAAAAAAAAAAAA
Mh Mwy wa CDM, Mh Katibu Mkuu, waheshimiwa wageni waalikwa ndani na nje, Asalaam Alaikhum, Bwana Yesu asifiwe, kristo- Tumaini letu.
Na ukawa pia UKAWAAAA-Tumaini letu.
Tunamshukuru Mwy Mungu kuepusha Mkutano Mkuu huu usifanyike

Rasimu baada ya kusomwa na wenzetu na kuona inasimamia misingi ya uwazi, ya uadilifu, walijaribu kuichakachua na kuinyoonga misingi ya katiba.
Bahati mzuri tulikuwepo na tunashukuru kulikuwa na muungano wa watu waliotaka misingi ya mawazo ya wananchi yanazingatiwa.
UKAWA Ukaanzisha msingi muhimu wa maendeleo ya nchi yetu.UKAWA unajenga kuaminiana miongoni mwa wa Tanzania, kwa kuheshimu mawazo ya wa Tanzania. UKAWA imejenga Trust.
Wenzetu wanaendelea na mchakato huo huku wakijua katiba haitapatikana, wanajaribu kutafuta kuhalalisha jambo hilo kwa njia yoyote, sisi tunasema kitendo hicho hakikubalikai, hakikubalikim hakikubaliki.
Ni muhimu vyama vyetu viendelee kushirikiana mpaka wakati wa uchaguzi ili tuweze tukapendekeza kwa pamoja nani mgombea wa urais wa pamoja, tuweze kushirikiana katika hatua zote.
Vyama sio mwisho ni kuweza kuwa na haki za kiuchumi, haki za kijamii, haki za kisiasa.
MAFISADI WANOKULA ELA ZA UMMA WAWEZE KUSHTAKIWA WAWEKWE NDANI WAFUNGWE.
Ni aiibu kwenye kila watoto 100 watoto 42 ni wadumavu. Bill Gates akija Tanz anashangaa akimuona mtoto huyu anaumri gani anaambiwa ana miaka 13, wakati anaonekana anamiaka 5.
Tufanye kazi ka pamoja ili rasilimali za nchi hizi ziweze kutunufaisha kwa pamoja.

Ninaiheshimu sana CDM kwani ndani yake kuna niliosoma nao, kuna waalimu wangu. kuna wangu mfano Prof Safari nilikuwa naye CUF na ninashukuru hakujiunga CCM amejiunga CDM , Kuna Mabere Marando nilikuwa naye enzi za kusoma kwangu n.k


Salaam kutoka kwa Prof. Lwaitama -akiwakilisha wasomi Nitasema mambo 2
1. MImi nawakilisha sio wasomi bali wana zuoni, hawa ni watu wanaotafuta maarifa na wapo wanazuoni wa aina 2, kuna wanaogundua majukumu ya kihistoria na wale wanaokuwa mamluki, wanajua majukumu ya kihistorias lakini wanajifanya kama hawafahamu.
Miaka ya 50 kulikuwa na vuguvugu la kujiletea uhuru na wanazuoni wa wahkati ule kuna walioingia mitini lakini wakina Jomo Kenyata, Kwame Nkruma, mna Nyerere walijumuika na kuangaika kjiletea uhuru.

Zama hizi ni zama za kujiletea ukombozi wa pili, Lumumba alilisimamia hili, na hili lilelezwa vizuri na TANU mimi nilijiondoa kwa TANU 1973.
Hizi ni zama za kungatua mamlaka, serikali 3 ni kungatua madaraka. Hizi ni zama la vuguvugu lingine na hili vuguvugu ni pamoja na watu wengine kama nyinyi CCM.
Mwaka 1977 tulikuwa na katiba, na 1979 katiba ya ZNZ je katiba hizi zinapelekea kuunga serikali moja? hapana serikali tatu
Jukumu kubwa ni lile lililounganishwa kwa neno moja UKAWA. 
CCM imechakachua mamlaka zake , na najua hata Mangula sio kama wao, wanamtumia tu. UKAWA sio chama ni vuguvugu, ni movement, kwahiyo msajili ukawa haitakiwi kusajiliwa ipo ndani ya vichwa vya watanzania. 



Dr Slaa
Waziri wa TAMISEMI wewe sio mtafsiri wa Katiba ya CDM, tuwaachie CDM wenyewe.
Kuna maeneo tuliyokosa kusimamisha viongozi wa serikali za mitaa kwa sababu ya tafsiri ya TAMISEMI.

Wakati tunaelekea 2015 kila kiongozi anawajibu kuhakikisha kuwa eneo lake anashinda, na kama kiongozi ni jukumu lako kuhakikisha unasimika mgombea.
Tunamuomba Rais kuwaweka watu kwenye sintofahamu nji jambo linalohatarisdha usalama wa nchi. Kutoeleza lini uchaguzi unafanyika ni kuwaweka wasiwasi watanzania, vyma vinashindwa kuwaandaa wagombea kwa sababu uchaguzi haujulikani.

2009 nilikabidhiwa kitabu chenye mipaka siku chache kabla ya uchaguzi, wakati CCM walikuwa na taharifa mapema, hujuma hii haitaendelea kuvumiliwa.

Mila potofu zinachangia kwa wakina mama kukumbana na hila na kushindwa kugombea. CDM mwaka huu tunafanya kwa matendo kwa kuhakikisha tunaandaa wakina mama wakutosha, kwenye vitongoji, madiwani nk. Ni lazima wakina maam tuwajengee mazingira.

2010 tuliunda Dira yetu ikiwa na misingi hii: uadilifu, umakini, na utu nashukuru Tume ya Warioba imeyachukua haya.
Rushwa iliyopo inatokana na kutokuwa na viongozi waadilifu.
Falsafa ya nguvu ya umma(Peoples Power) inasisitiza mamlaka ya kushika mamlaka ya kusimamia uchumi, kuamua juu ya mstakabali wa nchi yao yatakuwa ndani ya wananchi wenyewe.

Lengo la CDM ni kujiandaa kwenda kushika dola na kumuondoa CCM
Sio jukumu la CDM kusifia chama tawala bali ni kukemea pale wanapokosea. Waliahidi maiha bora kwa watanzania, ahadi isoyotekelezeka kwani wananchi wameanchwa na umaskini wa kutupwa

Mtakaporudi nyumbani mnapaswa kufanya kazi ya kumalizia kujenga chama kwa silimia 20 iliyobaki, tunawaraka tutawakabidhi na kuna ratiba na tunawataka mpaka kufikia JAN 2015 MUWE MUMEMALIZA ili Mangula asiweze kupumua. CCM hawatubabaishi leo hii tunamtandao kama 

Nataka nimwambie msajili leio kuwa kama ni kufanikiwa ni kufanikiwa kwenye kuwaunganisha watanzania, tumefanikiwa kwa asilimia 90, leo watanzania wamepata uhuru kwa kujua haki zao, hawaogopi mtendaji wa kijiji wala kiongozi yeyote wa serikali.

Gazeti la MwanaHALISI limefungiwa mpaka leo na hakuna sababu ya maana. Tunataka ieleweke kuwa haki za Waandishi wa habari zipo mashakani.

Kuna utata mwingi wa kadi ya kielektronic ya kupigia kura. Nyie viongozi mkitoka hapa siku itakavyotangazwa kupiga kura hakikisheni wananchi wanajiandikisha. Tutatoa ratiba ya utekelezaji.

Maandamano yamehamasisha uboreshaji wa huduma za wananchi, mfano tulimtaka Rais arekebishe bei ya sukari, tukampa siku 7 baada ya siku 6 akarekebisha na kuwa 1700/ japo haikutekelezwa.
Tusitegemee CCM kama itarekebisha masiha ya mtanzania, tunapaswa kuipiga chini.

Mauaji, Arusha, Igunga, Nyororo n.k Rais mpaka leo hajaunga tume ya kimahakama. Mh Rais tunarudia tunaushahidi askari aliyeuwa tunao, mnavyosingizia CDM wanausuka mnaogop anini kutushtaki.



Ruzuku 2011-2014 June Bilioni 8.4
Vyama Rafiki Milioni 642,323,635.47
Mikopo -Kwa niaba ya chama naomba niwamshukuru sana Freeman Mbowe, Ndesamburo, Grace Kiwelu NA Suzan Lyimo kwa ufadhili wao kwa chama. 


MBOWE Makamanda Peoplesssssssssssss, mnanitia aibu Peoplessssssssssssss-Powerrrrrrrrrrr

NIna kila sabau ya kumshukuru Mungu kwa siku ya leo. 
Chama kimeondokewa na viongozi waandamizi
Naomba nitambue kuwa katika kipindi hiki tuliondokewa na 
1. Bob Makani
2. Shinyaga
3. Rejia Mtema
4.. Mama Issa Salum
5. Kabigi
6. Mzee Waledi

Wanachama a viongozi wa ngazi mbalimbali waliotutoka napenda niwatambue.
Waliofariki kwenye mikutano halali ya harakati za ukombozi na uchaguzi

Denis Michael-Arusha
Ismail Omari Arusha
Paul Njuguna- Kenya mkenya aliyekuwa anapita tu masikini mauti yakamkuta
Ali Zona - Moro muuza magazeti
Mbwana Masoud-Igunga
Daudi Mwangosi- Aliuwawa kwa maelekezo ya RPC, na RPC huyu alizawadiwa kwa kupandishwa cheo
JUdith Mushi na watoto wengine 4 walikufa kwa niaba yangu kule arusha 16. 05. 2013, kwasababu waliudhuria mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani wa kata 4, ndugu wajumbe tusimame kwa dakika 1.

Machozi yenu na damu yenu iliyomwagwa haitapotea bure, Tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu.
TUnatambua familia zenu zinayoathirika, kazi hii ya mapambano inahitaji sucrifice, wakina mama hawaaonekanai, wakinababa hawaonekani. Lakini familia zetu zifahamu kazi hii tunayoifanya kukombo ataifa hili.
Tusiogope kwani makamanda wa Arusha, Lema ndugu yangu anasema dhambi kubwa kuliko zote ni Uoga.
Adui yetu leo ni dola ambalo halielewi ni jinsi gani wanainchi wanateseka. Mwakani viongozi hawa watakapokuja uraiani wataona ni jinsi gani wamehusika kudumaza hali ya wananchi. 

Nisikitike namna ambpo propaganda zinavyotumika kuchafua mashirika mabalimbali. CCM hawawezi ku survive bila misaada ya marekanio, misaada ya china, misaada ya uingereza, CCM ni ombaomba wanafikiri CDM nao ni ombaomba, sisi sio ombaomba watu wetu wanatupa pesa kwa kujenga uwezo wa viongozi wetu.
Ndugu wageni wetu kaielezeni dunia kuhusu CDM, kwasababu vyombo vyetu vya habari vinapotosha kwa kuandika kwa kupendelea serikali, tunataka vyombo vya habari visituandike kwa kutupendelea.
Vyombo vya habari visiandike kesho mbowe apata ulaji hapa akuna ulaji ni mzigo tu 

Historia ya CDM 1992 MKutano Mkuu-Edwin Mtei Mwy
Alijenga chama hiki kwenye mazingira magumu sana, lakini misingi aliyoijenga ndio iliyoifantya CDM ifike hapa.
Katika waasisi 36 wa kwanza waliobaki hawafiki 5
Tulikuwa tukifanya mikutano mikuu kama hii wajumbe wanalala majumbani kwetu, tuliijenga chadema katika wakati mgumu. 
Ni matumaini yangu namuomba mwenyezi Mungu Mabtia tutakuwa naye chama kimoja, Lipumba tutakuwa naye chama kimoja .....licheko
1994 - Madiwani 42 na wabunge 4 
1998- Bob Makani kama mwenyekiti
2000-Lipumba aliungwa mkono tukapaka wabunge 5 nmadiwani 72
2004-Mbowe kama mwenyekiti
2005-Wabunge 11 Madiwani 103
2009-Nikarekeshwa kama mwenyekiti (Mbowe)
2010-Wabunge 49 madiwani 572 wa kuchaguliwa na 200 wa viti maalumu.

- - - Updated - - -

Chama chetu kimekuwa kwa awamu, ari yetu na kasi yetu inachagizwa na serikali kuleta umaskini.
Mbowe anaendelea: Umasikini unaonekana kama sifa ndani ya CCM viongozi wake wanaona sifa kujitambulisha kama watoto wa masikini au watoto wa mkulima. Umasikini sio sifa na welkedi kama CCM wanavyofikirisha, wana CDM tusikubali umasikini, tusikubali kuuenzi wala kuukumbatia tuuchukie.
Isiwe lugha ya mwanachadema kuanzia leo tuutokomeze umaskini kwani ni laana.
Tujiandae kwa uchaguzi ujao huu kazi hii ni ngumu sio rahisi.
Ndugu zangu wanachadema naomba niwaambie mamluki wote hiki chama hamukiwezi



 Mbowe: Chadema ni mpango wa mungu, chadema ni muunganiko wa damu za watu, masikitiko ya watu.
Nashukuru Mungu chama hiki leo kipo salama kipo salama kuliko majamaa wanavyofikiria.
Chama cha siasa sio sifa ni fikra, ni kujenga fikra za watanzania juu ya kile wanachokitaka, chama cha siasa sio majengo sio ofisi ni fikra.


 Mbowe: Chama hiki hakina tatizo la wanachama chama hiki kina tatizo la viongozi kwenye maeneo yaliyo mengi.
KIla baada ya miezi 6 tutatathmini utendaji wa viongozi wetu huna taharifa za mikutano, huna michango tunakuondoa, OK? OK? isije baadae ikawa noma..



 Mbowe: Every cloud has a silver lining ...Mambo amabyo CCM walitufanyia bungeni na kutuona wanyonge tukaamua kuwa pamoja na wenzetu tukajuinhga nao na kuwa na umoja wa UKAWA. Ufisadi walioufanya bungeni umetupa manufaa kuwa na umoja wa UKAWA

 Lugha ya kuendelea na bunge Dodoma ni wizi, ni batili. Mwenyekiti wa bunge anakusanya maoni, anabadilisha kanuni amekuwa Warioba?



 Sasa naomba nitangaze tamko, mpo tayariiiiiiiiiiiiiiii. eeeeeeeh mpo tayariiiiiiiiiiiiiiiiiii



 Sasa ni vema tukawa na azimio la mkutano mkuu huu kuwa BMK lisitishwe mara moja na kama halisitishgwi tutachukua hatua zifuatazo.

 Kushirikisha umma kuwa na migomo isiyokuwa na ukomo kwa kibali cha polisi au bila kibali cha polisi

 Naomba niwaambie maamuzi tutakayofanya yana gharama kuna ambao watakuwa mstari wa mbele tutapigwa risasi. ninaagiza chama na kushirikiana na asasi za kiraia kuwaandaa wananchi kufanya mandamano yasiyokuwa na kikomo

Kila mmoja akitoka hapa kila Wilaya ije na mkakati wake wa kushirikisha raia jinsi watakavyoandaa maandamano.
Kwa kanda ya kati waandae matamko kuonyesha kinachofanyaika Dom ni ubatili

 Kanda ya KATI MAANDAMANO YALENGE ENEO LA BUNGE.

 Hatua nyingine za mkakati zitatangazwa. Kila mmoja aende wilayani kwake na arudi na mkakati haraka, tunajua watatumia dola lakini hamna taifa lililopata uhuru bila ya hatrakati


Jumuiya ya kimataifa tunaomba mtuelewe tunauchungu kwa nchi hii tunaomba mtuelewe. 





MATOKEO RASMI:

Uchaguzi mkuu umefanyika kwa amani kabisa na yafuatayo ndiyo matokeo rasmi:

Makamu Mwenyekiti zanzibar

Said Issa Mohamed 645
Hamad Mussa Yusuph 163

Makamu Mwenyekiti Bara

Professor Abdallah safari 
Kura za Ndiyo 775
Kura za Hapana 34
Zilizoharibika 2

Mwenyekiti Taifa

Freeman Aikael Mbowe 789
Gambaranyera Mong'ateko 20
Zilizoharibika 2

Ushindi wa Freeman Mbowe ni asilimia 97.3%

Sasa ni Rasmi Freeman Mbowe ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi cha tatu cha mwaka 2014-2019



BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com