Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIKUNDI CHA MAZINGIRA CHA CHAMAGUHA SEKONDARI CHATOA MSAADA KITUO CHA WALEMAVU BUHANGIJA SHINYANGA

Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na wasioona zaidi ya 270 ,kituo cha Buhangija Jumuishi ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita wanakikundi wa asasi ya kijamii Shinyanga Ecological club( Kikundi cha Mazingira kutoka shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga) walitembelea kituo hicho na kutoa elimu ya utunzaji mazingira,kutoa msaada wa chakula,nguo,vifaa vya kufanyia usafi na sabuni kwa watoto hao.Pichani ni mwalimu mlezi/ mratibu na mwanzilishi Ezra Manjerenga akigawa sabuni za kufulia kwa watoto hao
Mratibu na mwanzilishi  wa kikundi cha Mazingira katika shule ya sekondari Chamaguha Ezra Manjerenga akigawa vifaa vya kufanyia usafi katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija Jumuishi mjini Shinyanga
Watoto katika kituo cha Buhangija wakiwa katika eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinajiri,ambapo pamoja na mambo mengine walisema kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kufanyia usafi

Zoezi la utoaji vifaa vya kufanyia usafi likiendelea.Hata hivyo wanafunzi hao mbali na kutoa misaada hiyo kituoni hapo, pia walitoa elimu ya Mazingira kwa watoto hao,kuhusu namna ya kuyatunza na kufanya usafi ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kutunza afya zao.
Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi cha Mazingira katika shule ya sekondari Chamaguha, Mohamed Ahmed akitoa elimu kwa vijana wa Buhangija mbinu ya umwagiliaji na utunzaji miti dripping watering method. Pichani pia ni wanafunzi wa Buhangija wakiwa wameuzunguka mche wa mti.
Wanakikundi cha Mazingira kutoka shule ya sekondari Chamaguha wakiendelea kutoa elimu juu ya utunzaji mazingira.Mwenyekiti wa kikundi cha Mazingira katika shule hiyo Chamaguha, Mohamed Ahmed, alisema kikundi chao kimejijengea tabia ya kusaidia watoto wasiojiweza kwa kuchangishana fedha na kile kinachopatikana huamua kusaidia watoto wenzao wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mazingira katika shule ya sekondari Chamaguha, Mohamed Ahmed akitoa elimu juu ya namna na kumwagilia maji miche ya miti

 Mwenyekiti wa kikundi cha Mazingira katika shule ya sekondari Chamaguha, Mohamed Ahmed  akigawa nguo kwa watoto wa Buhangija mjini Shinyanga

Mratibu na mwanzilishi wa kikundi cha asasi ya kijamii Shinyanga Ecological Club  tawi la Chamaguha Sekondari bwana Ezra Manjerenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto katika kituo cha Buhangija Jumuishi mjini Shinyanga

Picha na maelezo yote na Marco Maduhu-Malunde1 blog-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com