KUHUSU MAHAKAMA-PISTORIUS HAKUKUSUDIA KUUA MPENZI WAKE

Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baada ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post