1. ACHA KUWA NA MARAFIKI
WANAOKUPOTEZEA MUDA Watu wengi tumekuwa na marafiki wengi sana na marafiki ni mhimu sana katika maisha yetu haya wapo wanaotufaa na wasiotufaa kuwa na marafiki wanao weza kukusaidia na kukupa hamasa ya kimaendeleo ,malengo yako na kuwa na maisha Fulani. Hivyo achana na marafiki wasio kuwa na msaada kwako.
2. ACHA KUKIMBIA MATATIZO YAKO
Waswahili wanasema kuwa “kukimbia tatizo si kutatua tatizo” Hivyo basi kama tatizo umekutana nalo basi tafuta njia ya kulitatua tatizo hilo kwani matatizo hayaji kuisha katika dunia hii kama unakimbia utakimbia mangapi ? Unatatizo la pesa kwanini usitafute pesa ila kama hufanyi kazi unategemea kupata pesa huwezi. Matatizo hayaepukiki komaa na ulitatue utajikuta kama uko peke yako katika hii dunia lakini kuna watu wana matatizo zaidi yako na wanahangaika kuyatatua.
3. ACHA KUJIDANGANYA MWENYEWE
Katika maisha ya sasahivi unaweza kumdanganya mtu yeyote yule lakini ogopa sana kujidanganya. Vijana wengi tumekuwa tukijivuna mbele za watu kuwa tuna hili mara lile ili mradi tu tuonekane ni watu wazuri kwa watu wanao tusikiliza.
4. ACHA KUIGA MAISHA YA WATU
WENGINE Vijana wengi hili kwetu limekuwa janga kubwa sana maisha yetu yamekuwa yakuigiza sana (copy and paste) hasa hasa tunapenda kuonekana ni watu Fulani wenye maisha mazuri, hatuzijui shida ni watu wakula bata wakati si kweli. Maisha yetu yamekuwa magumu na yatakuwa magumu kwasababu ya kuiga maisha ya watu wengine ishi maisha halisi uliyonayo watu wakajua asili yako siyo kuigiza unaweza kosa kusaidiwa na watu.
5. ACHA KUKUMBUKA YALIYOPITA
Hapa kuna mambo mengi tunajifunza wengi hukumbuka yaliyopita hasa waliyo shindwa kuyafanya au yaliyowaumiza kwa kukumbuka yaliyopita haiwezi kukusaidia kwani kila tuamkapo asubuhi ni kama tumezaliwa upya na siku ni nyingine,tarehe na mambo utakayoyafanya ni mengine si sawa na jana. Waswahili wanasema “Tusahau yaliyopita tugange yajayo” hii ina maana kuwa wewe si wa kipindi kile bali ni mwingine na akili ni mpya.
6. ACHA KUOGOPA KUFANYA MAKOSA
Makosa ndiyo walimu wetu mkubwa sana katika maisha yetu na kila binadamu si mkamilifu toka uzaliwe mpaka sasa kuna makosa mengi uliyoyafanya na kupitia makosa hayo umejifunza kutorudia makosa tena na makosa hutujenga zaidi na kuwa makini zaidi kama ukifanya kosa huna haja ya kujilaumu chukua muda kujilekebisha na kusonga mbele kosa lisiwe tatizo la kukukatisha tamaa.
7. ACHA KUNUNUA FURAHA
Vitu vingi tunavyo vihitaji vinagharama kubwa sana na vitu hivyo si kwamba tuna vipenda bali ni tamaa tu tuliyonayo na hiyo yote ni kuamini kuwa furaha ya maisha tutaipata huko si kweli. Mungu alitupatia furaha, na upendo bure ni vitu unavyozaliwa navyo fikiria kama vingekuwa vinauzwa wangapi? Wangapi tungekuwa hatuna furaha. Hivyo basi anza kuyafurahia maisha yako hivyo vingine vitakufuata.
8. ACHA KUSHINDANA NA MTU
KIMAISHA Acha kushindana na mtu kimaisha haitakusaidia huwezi jua yeye anafanya nini kuzipata pesa zake au mali zake na wewe unazipataje ushindani mzuri katika maisha ni ule wa kwako na mafanikio yako jiangalie kile unachokifanya na matokeo yake unapata nini? huo ndio ushindani mzuri kuliko wote sio kushindana na mtu kimaisha acha.
9. ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO
YASIYO SAHIHI Katika mahusiano si kitu cha kujiingiza tu au kama unaoa si kuoa tu kwasabu Fulani kaoa basi na mimi nioe, si kudai kuwa nimechoka kufua ngoja nioe sasa ndiyo maana karne hii inaongoza kwa wanandoa kuachana na ndoa za utotoni kwasababu watu hawajipangi ni kuiga tu. Mahusiano au ndoa ni kitu kikubwa sana na kama umempenda mtu onyesha kuwa unampenda kweli mtangulize mbele yako kuwa ndiyo kila kitu kwako/ kila kitu kinaenda kwa ajiri yake. Kama unaingia katika mahusiano mheshimu mwenzako na kumpenda mpe nafasi kubwa katika maisha yako.
10. ACHA KUJILAUMU
Kuacha kujilaumu ni njia mojawapo ya kufanikiwa katiaka maisha yako unapo kosea amini kuwa wewe si mkamilifu na hakuna binadamu aliyekamilika jipange songa mbele. Wagunduzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kama vya umeme na vinginevyo si kwamba hawa kufanya makosa walikosea sana mpaka kutoa kitu sahihi .
11. ACHA KUONGELEA YA WATU FULANI.
Kuzungumzia maisha ya mtu Fulani haikusaidii ni kupoteza muda tu kwanini usiwaze maisha yako unatakiwa kufika wapi na ufanye nini kuishi maisha mazuri unakaa na kuanza kuzungumzia mtu Fulani yupo hivi mara hivi wakati huo huyo mtu unaemsema yeye yupo kazini we upo kijiweni mtalingana kweli? Acha kuzungumzia maisha ya watu fanya yako ufurahie maisha. Bonyeza maneno haya Tukutumie habari zetu zingine zenye kukusaidia katika maisha yako |
Social Plugin