Watu kumi wamefariki dunia baada ya kukakanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki.
Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo nchini Afrika Kusini wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu hiyo angalau kujipatia kipande cha nyama.
Msemaji wa polisi aliambia shirika la habari la AFP kwamba mnyama huyo aligongwa na wanakijiji wakaona fursa ya nyama ya bure ambapo walikimbia kuinyakua na kuanza kuikatakata, ''
''Hapo ndipo gari lililokuwa linakwenda kwa kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata nyama hiyo na kuwaua,'' aliongeza kusema msemaji huyo wa polisi.
Watu wengine wawili walifariki kutokana na majereha yao mabaya wakiwa wanapokea matibabu hospitalini.
Polisi wanasema kuwa watu wengine saba akiwemo dereva wa gari hilo wanapokea matibabu hospitalini.
Social Plugin