Samaki aina ya Goldfish, anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji kutolewa uvimbe kwenye ubongo wake.Upasuaji huo umesemekana kufanywa kwa uangalifu mkubwa kutokana na hofu yatisho kwa maisha ya Samaki huyo.Samaki huyo kwa jina George, ambaye mmiliki wake anaishi Melbourne, alidunguwa sindano ya kuondoa fahamu iliyogharimu dola 200.
Daktari Tristan Rich, aliyefanya upasuaji huo, aliambia kituo cha redio cha 3AW mjini Melbourne kuwa Samaki huyo kwa sasa amepata fahamu na tayari ameanza kucheza na kuogelea majini.
Wataalamu wa matibabu ya wanyama, wanasema kuwa Samaki huyo mwenye umri wa miaka 10, anatarajiwa kuiishi kwa miaka mingine 20.
“George alikuwa na uvimbe mkubwa sana kwenye ubongo wake na alikuwa anakuwa polepole sana, na hali hiyo ilikuwa inaanza kuathiri maisha yake,” alisema daktari Rich kutoka hospitali ya matibabu kwa wanyama ya Lort Smith.
Mmiliki wa George, alikuwa ameambiwa achague kati ya Samaki huyo kufanyiwa upasuaji au adungwe sindano ya kulala.
Lakini aliona bora kujaribu kuokoa maisha ya Samaki wake na ndipo akakubali Samaki huyo afanyiwe upasuaji.
Aliongeza kuwa Samaki huyo alisalia kuwa hai kutokana na madaktari kuweka hewa ya Oxygen kwenye maji wakati wa upasuaji.
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA
BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA