HIP HOP GOSPEL SASA YAENDELEA KUWA KINARA KATIKA MUZIKI WA INJILI ALFREDY FUNDA ni mwimbaji wa mziki wa Gospel Flavour kutoka kundi kubwa la INJILI NI MOTO USIOZIMIKA lililopo jijini Dar es salaam.
Msanii huyu aliwahi kutamba na nyimbo ya JIFUNZE UPENDO kwa baadhi ya media sasa ameamua kuja mzima mzima na nyimbo yake kali sana inayokwenda kwa jina la ACHA KUMBIP MUNGU ambayo imekuwa gumzo katika matamasha na mikutano jijini Dar es salaam kwani ameanza kuachia baadhi ya media jijini Dar es salaam.
Ameimba kwa staili ya tofauti sana miondoko ya soft HIP HOP amekuwa akiwakamata mashabiki kwa meseji yake watu wenye tabia ya kumbip mungu .
tulijaribu kumuuliza alifikiria nini juu ya huu wimbo ,lakini alidai mungu amempa ufunuo.
"Niliamka nikiwa na kiitikio cha kumbip mungu KWANI vijana wengi au binadamu tunambip sana mungu SASA HII NI SINDANO YAO UKWELI NA UWAZI",alijibu
Ameongeza kwa kusema video ya wimbo huo inakuja ipo katika maandalizi mazuri na ya kisasa.
Anaongeza kuwa "Watu wanatuita walokole washamba sasa watajua kuwa wao ni washamba sisi tupo town tuna afya nje na ndani.
Wasiliana naye kwa simu namba 0714142384 ,Email-alfrredyfunda@gmail.com ,anakaribisha mialiko kwani timu ya INJILI NI MOTO USIOZIMIKA [IMU] Ipo sambamba naye MBARIKIWE SANA
SIKILIZA HAPA CHINI WIMBO WA "ACHA KUMBIP MUNGU"
Social Plugin