Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENGE WA UHURU KUTUA SHINYANGA KESHO KUTWA, MIRADI 58 KUZINDULIWA




Mkoa wa Shinyanga utapokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Geita tarehe
01 Oktoba 2014 katika kijiji cha Mwabomba,Kata ya Idahina, Halmashauri
ya Wilaya ya Ushetu Wilayani Kahama na utakimbizwa kwa siku sita kabla
ya kukabidhiwa Mkoani Tabora Tarehe 07/10/2014 katika kijiji cha Nata
Wilaya ya Nzega.



Mwaka huu 2014 Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Shinyanga utapitia jumla
ya miradi 58, ambapo miradi 5 itazinduliwa, 20 itafunguliwa, 13
itawekewa mawe ya msingi na miradi20 itaonwa. Miradi yote ina thamani
ya Sh. 10,378,951,014.

Gharama za miradi yote hii imetokana na nguvu za wananchi,
Halmashauri, Serikali Kuu na Wahisani mbalimbali.



Ratiba ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu mkoani Shinyanga itakua kama ifuatavyo:
Tarehe 01/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Tarehe 02/10/2014 – Halmashauri  ya Mji Kahama
Tarehe 03/10/2014 –Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Tarehe 04/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Tarehe 05/10/2014 – Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na
Tarehe 06/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu



Mwenge wa Uhuru hukimbizwa kila mwaka katika Halmashauri zote nchini
kuanzia mwezi Mei hadi Oktoba kuhamasisha wananchi, mashirika, taasisi
na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu zao kuchangia kwa hali na mali
kufanikisha miradi miradi ya maendeleo waliyobuni wenyewe katika
maeneo yao kulingana na fursa zilizopo na mahitaji yao halisi.



Hivyo, Wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga wanahimizwa kujitokeza
katika maeneo yote Mwenge utakapopita ili kushuhudia utekelezaji wa
shughuli mbalimbali za maendeleo walizoibua wenyewe.



Ujumbe wa Mwenge Mwaka huu ni ‘Katiba ni Sheria Kuu ya nchi, Jitokeze
kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com