Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIAMOND PLATNUMZ WA TANZANIA SASA KUFANYA SHOW YA BURE SEPTEMBA 20,2014 NCHINI UJERUMANI

Mwishoni mwa mwezi uliopita msanii anayewakilisha vyema taifa lake la Tanzania Diamond Platnumz alikuwa anafanya show kubwa mjini Stuttgart,Ujerumani na show kushindikana kufuatia vurugu kubwa katika ukumbi ambapo chanzo cha vurugu hizo ni kutokana na Diamond kuchelewa kupanda jukwaa.


YES!!!! STUTTGART GERMANY!!! on this 20th of September 2014... kiukweli nilisikitishwa sana na kilichotokea last time Stuttgart... lakini baada ya kugundua kuwa pia lilikuwa ni kosa la mtu mwingine na si promotter kama nilivyodhani, yaani Brittis Events.ndipo tulipoamua na kuwaletea Burudani hii Mashabiki zetu pendwa wa Stuttgart....hakikisha ufikapo unapendeza zaidi maana kama ujuavyo safari hii Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi vitakuwa pale kwa RedCarpet.... kiingilio ni BUREEEEEE!!!... tafadhariwambie na wenzio wa nchi za karibu...#NORWAY #HOLLAND #SWITZLAND #BELGIUM #SWEEDEN na kadharika!!!! Aliandika Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Facebook.


Kwa kilichopangwa na waandaaji wa show hiyo ni kwamba show hiyo itafanyika tena na mara hii show hiyo itakuwa ni bure kama fidia kwa mashabiki wa burudani na mashabiki wa muziki wa Diamond Platnumz ambapo tarehe ya kufanika kwa show hiyo ni tarehe 20 Septemba mwaka huu.

TUNAPENDA TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA, LIKE PAGE YETU SASA HIVI UENDE NA WAKATI. BONYEZA HAYA MANENO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com