TAARIFA KAMILI KUHUSU SAKATA LA NESI KUDAIWA KUCHANGIA KUUA WATOTO MAPACHA WODINI,HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Dkt Ntuli Kapologwe kuhusu sakata la nesi kudaiwa kuchangia vifo vya watoto wawili mapacha kutokana na kile kichodaiwa kuwa nesi alikuwa bize na simu.Dkt Mlekwa amesema wamebaini kuwa mimba ilikuwa na miezi 6 na ilikuwa imeharibika na kwamba,mama anayedaiwa kujifungua ana miaka 15,mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Mwasele.Dkt Mlekwa ameongeza kuwa watoto waliozaliwa mmoja alikuwa na uzito wa gramu 500,wa pili gramu 700 ambapo kimsingi hawawezi kuishi na kwamba nesi aliyetupiwa lawama alikuwa ameshawapa taarifa ndugu wa binti kuwa mimba imeharibika lakini hawakutaka kuelewa.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Binti aliyejifungua watoto mapacha,ambaye amekiri kujifungua watoto wadogo sana tofauti na watoto wengine wanaozaliwa.Amesema alijifungua mtoto wa kwanza mdogo sana akiwa amekufa na wa pili akiwa hai lakini alifariki baadaye.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BOFYA HAPA KUONA PICHA,HALI ILIVYOKUWA JANA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA


BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI MARA MOJA ILI TUKUTUMIE HABARI ZETU ZOTE KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post