|
Ni siku ya kama ya tatu leo mjini Shinyanga kumezuka kitendo cha Shirika la umeme nchini kukata kukata umeme kila dakika hali ambayo imeleta hofu kwa wateja wa shirika hilo kuunguziwa nyumba na vitu vyao.
Wakizungumza na malunde1 blog wakazi wa Shinyanga wameeleza kukerwa na tabia ya TANESCO kukata umeme ovyo kila dakika na kurudisha tena bila hata kutoa taarifa ya kwanini wanakata na kurudisha.
Hata hivyo Kaimu Meneja Tanesco mkoa wa Shinyanga
Arthur Gama amesema kata kata hiyo ya umeme inatokana na pale mafundi wanapokuwa wanafanya
marekebisho ya hitilafu, na kujaribu kama tatizo hilo limetengemaa na hivyo
wanazima wanawasha.
Amesema kuna tatizo
limetokea katika line ya kusafirisha umeme maeneo ya viwanda, mtaa wa Matanda
mjini Shinyanga tangu juzi na wanaendelea na matengenezo
HISIA ZA WANANCHI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
+++++++++
TANESCO shinyanga hivi mmeanza kucheza kamali na wananchi? Huo umeme wenu wakamali toka juzi ni nin? kama mko kwenye ufundi kwanini msizime jumla au mtoe tangazo tujue maan mimi siwasomi kabisa huu umeme ndani ya lisaa moja unakatika mara4 jamani ni komborela kuwa mnatutambia mmejitokeza au mmejificha tuwatafute? Acheni basi utani na mali za watu nini maan ya TANESCO TUNAKUANGAZIA MAISHA YAKO au ni kinyume TUNAKUUNGUZIA MAISHA YAKO? binafsi nimechukia mno cjui wew mwana shy mwwnzangu
|
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Tanesco si bora mkate umeme moja kwa moja siyo kukata kata hovyo,utaratibu gani huo dakika 5 mnakata,mara sekunde 40 mnarudisha..NI shinyanga tu au na mikoa mingine!?
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com