Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANABUSEGA WALAANI TUKIO LA MWALIMU KUBAKWA NA MAJAMBAZI HUKO SIMIYU

Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (Budeco), imelaani tukio la kubakwa mwalimu wa shule ya Busega mkoani Simiyu.
Tukio hilo lililotokea Agosti 23 mwaka huu, ambako majambazi wakiwa na silaha walivamia nyumba ya Mratibu Elimu Kata, Samwel Mkumbo na kupora sh milioni 18, kisha kuvamia chumba cha mpangaji ambaye ni mwalimu wa kike na kumpora sh 50,000 na kumbaka.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi,

Mwenyekiti wa Budeco, Massele Ginhu, alisema tukio hilo litarudisha nyuma maendeleo ya elimu, kwa kuwa ni moja ya changamoto inayowakabili wilayani hapo.

Alisema kitendo hicho si cha kufumbiwa macho na wahusika watakaobainika, wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo vya kinyama na kiuaji kwa watu wanaojitolea kufanya kazi ya kujenga taifa.
Aidha, wanachama wengine wa Budeco walishauri serikali kujenga nyumba karibu na mazingira ya kazi ili kulinda wafanyakazi na watumishi wa umma wanaofanya pembezoni mwa miji.
Pia, walishauri ulinzi shirikishi kuboreshwa ikiwa ni njia ya kusaidia kulindana kwa watu wa maeneo yenye matishio ya uhalifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com